MUIGIZAJI na mchekeshaji maarufu bongo
Steven Nyerere, amesema anatamani kukutana na Rais Magufuli amshauri
azime data, ili watu wasitumie mitandao ya kijamii kwa kufanya umbea na
kuongea habari za uongo za kuchafuana.
Akizungumza na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema iwapo
atapata fursa hiyo atamsahuri Rais Magufuli kufuata wanachokifanya
China, ambapo wao wamepiga marufuku utumiaji wa mitandao ya kijamii
mbali mbali, na kutumia mitandao mingine ya kwao kwa ajili ya kukuza
uchumi wao na sio kwa ajili ya kupiga umbea na kueneza habari za uongo.
“Bado tunahitaji kuwa na mwenendo wa China, nitafurahi sana
siku Magufuli akizima data, na nadhani kuna haja ya kumshauri
Mheshimiwa Rais, kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda,
ni lazima siku moja tuzime data hata mwezi nadhani tutafikia malengo,
tena andika kabisa Nyerere anatamani kuonana na Magufuli amnong'oneze
kuhusu data, azime tu hata nwezi, ili watu wafanye kazi, amesema Steve
Nyerere.
Steve ameendelea kwa kusema kwamba ….. “asilimia 90
wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi taifa hata
pato, nia ni kuliongezea taifa pato, wenzetu China wameendelea kutokana
kutoipa nafasi mitandao kuihairbu China yao, wameipa nafasi kwa ajili ya
kutangaza biashara na utalii, sasa sisi tumeipa nafasi kwa jili ya
umbea”,.
Steve Nyerere ametoa kauli hizo zote kutokana na watu
kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia, baada ya kugundua amezaa nje
ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.
0 Comments:
Post a Comment