Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Omari Matonya
anatafutwa na jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuwaua kwa
kuwachinja mke wake na mtoto wao, kisha kukimbia.
kamanda wa Polisi mkoa wa
Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kwamba mtu huyo amefanya tukio hilo
nyakati za usiku wakati wakiwa wamelala, huku chanzo kikubwa kikitajwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi.
“Mwanamke ambaye anaitwa Moshi Daudi mwenye miaka 24 akiwa
na mtoto wake wa mwaka mmoja anayeitwa Omari Matonya, waliuawa kwa
kuchinjwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mwanaume anaitwa Omari
Matonya mwenye miaka 25, ambaye ni mume wa huyo mama na baba mzazi wa
huyo mtoto, baada ya kufanya tukio hilo alitoweka. Alifanya tukio hilo
wakati familia yake ikiwa imelala na chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa
mapenzi, ambapo huyo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa na mahusiano na
shemeji yake, ambaye ni ndugu yake huyo Matonya anayeitwa Lazima
Matonya”, amesema Kamanda Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amesema mpaka sasa hajapata taarfa zake
zozote na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta, ili afikishwe kwenye
vyombo vya sheria.
SOURCE eatv

0 Comments:
Post a Comment