BAVICHA WACHARUKA SAKATA LA LISSU, WASIMAMISHA VIGOGO WAWILI


BARAZA la Vijana Chadema, (BAVICHA) limelitaka Jeshi la polisi na vyombo vya usalama nchini vikiri kushindwa kumpata aliyemjeruhi kwa risasi mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu na waruhusu vyombo vya kiuchunguzi vya nje kufanya kazi hiyo.

Aidha wamewafukuza uanachama aliyekuwa Makamu katibu mkuu wa chama hicho Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Kilimanjaro, Dickson Kibona kwa kufanya vitendo ambavyo ni utovu WA nidhamu.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi ameyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mara baada ya kumalizika kikao cha kamati Tendaji  ya baraza hilo akiwa viongozi ameambatana na viongozi.

Alisema kuwa imepita miezi nane tokea Lissu ashambuliwe kwa risasi zaidi ya 38 na mpaka sasa jeshi la polisi wameshindwa kumkamata muhusika hivyo akashauri ni vema wachunguzi wa nje ikiwemo wale wa UINGEREZA scottlandyard wakashirikishwa ili ahusika wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Amesema sababu za kuwafukuza uwanachama Ndibalema na Kibona ni kuwa walithibitika kuwa walikuwa wakipinga hadhani maamuzi halali ya vikao vya chama na walipopewa nafasi ya kujieleza mbele ya tume iliyoundwa kuchunguza suala hilo, Ndibalema alijiuzulu huku Kibona akigoma kupokea barua ya Tume.

0 Comments:

Post a Comment