MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) Freeman Mbowe ametuma ujumbe mzito wa Pasaka kutoka kwenye gereza Segerea.
Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai na kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni anashikiliwa pamoja na viongozi wengine wakuu akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vicent Mashinji, na Manaibu wake John Mnyika na Salim Mwalimu, na wabunge Peter Msigwa na Esther Matiko .
Viongozi hao wanaendelea kusota rumande licha ya kuwa wamepewa dhamana na mahakama baada ya askari magereza kudai kuwa gari lililowabeba kuwapeleka mahakamani Machi 29, mwaka huu liliharibika likiwa njiani hivyo kushindwa kuwafikisha washitakiwa hao hivyo kulazimika kuendelea kusubiri mpaka Aprili 3,mwaka huu ambayo ni siku ya kazi.
Mbunge wa Rombo alienda kuwatembelea viongozi hao Machi30, mwaka huu ambapo alimnukuu Mbowe akisema, "Tuko imara, tuko vizuri. Wapelekeeni wenzetu ujumbe huu. Msiogope. Taifa linatutegemea. Chadema ndiyo pekee itakayobadilisha uonevu unaofanywa na watawala kwa watanzania na kuwajakikishia demokrasia, amani ya kweli, haki na maendeleo.
Tukiwa waoga tutakuwa wasaliti wa matamanio hayo ya watanzania." .
Selasini alisema kuwa Mbowe na viongozi wengine wamemweleza kuwa wamepata muda mzuri wa kupumzika na kufanya retreat(tafakari ya kina,” Tumemkuta Mwenyekiti Mbowe akiwa na Biblia mkononi. Amesema amesoma na karibu anamaliza injili zote. Pia yeye pamoja na Mchungaji Msigwa leo wataadhimisha ibada ya ijumaa kuu kwa kuwashirikisha mahabusu na wafungwa wote wao kama watumishi wa neno la Mungu,”.

0 Comments:
Post a Comment