JPM AMWAGA AJIRA WAJENZI UKUTA MERERANI



Akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ukuta huo,Mapema leo katika kijiji cha Naisinyai ,Mererani ,wilayani Simanjiro ,mkoa wa Manyara,Rais Magufuli amesema kimsingia hana cha kuwalipa vijana hao  ila atahakikisha wanapata ajira kupitia majeshi yote yaliyopo hapa nchini.

"Navishukuru vikosi vyote vya  Operesheni cha Jakaya Kikwete na cha John Magufuli ,Mimi sina cha kuwalipa,Ila kuwalipa kwangu ni kuhakikisha mnapata ajira kupitia majeshi yetu" Amesema Magufuli.

Awali Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Nchini JWTZ,Jenerali Venance Mabeyo alimwomba rais Magufuli kuangalia uwezekano wa kulipa fadhila Kwa vijana hao walioshiriki Ujenzi wa Ukuta huo uliogharimu kiasi cha shilingi billion 5.65  hadi kukamilika kwake.

0 Comments:

Post a Comment