JPM ATOA MILIONI 100 KWA MGUNDUZI WA TANZANITE

Rais, John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia shilingi Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma zimsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

Amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako amezindua Ukuta uliojengwa kuzunguka Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.

“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.," amesema Rais Magufuli na kuongeza...

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,”.

0 Comments:

Post a Comment