Mahakama nchini Kenya imewahukumu Waziri wa Usalama, Fred Matiang'i, Mkuu wa Uhamiaji, Gordon Kihalangwa na Mkuu WA POLISI, (IGP) Joseph Boinnet kulipa faini KSh200,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 4.4 za Tanzania kwa kosa la kuidharau mahakama.
Jaji wa Mahakama Kuu, George Odunga Jumatano alisema viongozi wamekaidi maagizo ya mahakama yaliyowataka kumuachia huru Dk Miguna Miguna.
Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani siku ya Jumatano lakini hawakufika ndipo akawapiga faini kwa kosa la kukaidi amri ya mahakama.

0 Comments:
Post a Comment