HIKI HAPA WALICHOONGEA WABUNGE WA CHADEMA EU


WABUNGE na Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) wametoa msimamo pamoja na kueleza sababu za msingi zilizowapeleka kwenye ofisi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, (EU) jijini Dar es salaam leo.





Leo tarehe 29 March 2018 kwa pamoja Wajumbe wa kamati Kuu na  wabunge wa Chadema tumeweka kumbukumbu sawia ikiwa ni Hatua ya Mwisho ya Utunzaji wa Kumbukumbu za Matukio kabla ya kufanya Hatua ya Mwisho ya kupambania Hadhi,Utu,Haki,Demokrasia na Ubinadamu.


Sisi Siwaoga hata Kidogo,Na Hatuto ogopa kukaa kwenye Nchi yetu na kuendelea kufanya siasa kwa Mujibu wa Katiba na Sheria kama wenzetu wachache wanavyotaka.wala hatukwenda kulialia,au kutia huruma.

Sisi tuna Njia nyingine nyingi  ya kupambania Haki,utu na Demokrasia ya Nchi yetu.

Kabla ya Kufanya lolote, leo tumepeleka ushahidi wa Matukio yote kwa Mlolongo,Matukio ya Kuchokozwa Kwa Makusudi na Serikali na Vyombo Vyake Vya Dola.

Nina Imani ya kuwa Mabalozi wametusikia na Wametuelewa kwa Upana zaidi Kwa njia hii kubwa ya kidiplomasia,sababu leo wameona Matukio yote,wameona Wabunge waliofungwa miezi sita na  wakashinda rufaa,Wameona wabunge waliofungwa kwa Hila za kukosa Dhamana,Na mwisho wakaona  Serikali Yenye Magari zaidi ya Laki 1 imekosa gari ya kuwachukua Mahabusu  Segerea sababu ya kumkomoa Mbowe na Wenzie.

Na sasa Ni Imani yangu kuwa Lolote Tutakalo Azimia Katika Mkutano Mkuu na Kamati kuu Chadema dhidi ya Kujilinda na Hali hii na kukomesha Matendo haya dhidivya chama Chetu,Viongozi Wetu na Wanachama wetu,JUMUIYA UMOJA WA ULAYA na Mabalozi wote wa ULAYA watatuelewa vizuri sana.

HAKI UNINUA TAIFA
Hakika Tutashinda.

Boniface Jacob
Mjumbe kamati kuu CHADEMA

0 Comments:

Post a Comment