Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli leo Septemba 10 2017, amemteua Prof Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji mkuu wa Tanzania.

Kushoto Prof Ibrahim Hamis Juma akiwa na Rais wa Tanzania, Mhe Dkt John P. Magufuli
Kabla ya uteuzi huo Prof Ibrahim Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo iliyoachwa na Jaji mstaafu, Mohamed Chande.
Shughuli za kuapishwa kwa Jaji mkuu mteule, zitafanyika kesho Ikulu jijini Dar es salaam na Rais John P. Magufuli.

0 Comments:
Post a Comment