"Habari, Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa Saba hapa Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale airport na matibabu yalianza Mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital. Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa theatre. Tangu Jana alipofika alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio. Hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri. Nitawajuza atakapo toka theatre. Chakushangaza hadi sasa tangu tuwasili hatujapata ushirikiano wowote wa ubalozi wa Tanzania hapa Nairobi, Si kwa balozi au maafisa wowote wale wa ubalozi. Mh Freeman Mbowe amezungumza na vyombo mbali mbali vya habari pia taarifa yake itatoka punde.
Hemed Ali
Mkuu wa Idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.
HABARI NJEMA KUHUSU MH. LISSU.
Mh Tundu Lissu ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya Masaa 7 tangu saa nne asubuhi hadi sasa saa kumi na Moja jioni na upasuaji umefanyika kwa mafanikio hivyo yupo Executive ICU kwa uangalizi wa karibu zaidi. Tutaendelea kuwajuza. Na tunawahakikishia kuwa madaktari wametueleza hakuna tishio lolote kiafya yuko macho na fahamu zote na hii ndio ilikuwa hatua ngumu na mungu ametupitisha hivyo tuendelee kumuombea apone haraka.
Hemedi Ali
Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.
MWENYEKITI MBOWE ASEMA JUU YA WALIOMPIGA TUNDU LISU
"Sasa gun fire inayotokana na Mashine gun kwa kawaida Risasi Ishirini na moja kwa MTU mmoja so jambazi.
Jambazi anaua mtu kwa risasi moja au mbili hana sababu ya kumumimia risasi asiondoke na chochote not even a Laptop.
Kulikuwa na kusudio la kisiasa kwenye jambo hili, na ni lazima hofu yetu kwanza iende kwa wale wamekuwa ni mahasimu wa chama chetu
Wamekuwa mahasimu wakubwa Mhe, Lisu wamekuwa wahasimu wakubwa Wa demokrasia Wa nchi yetu".
Source BBC Swahili



0 Comments:
Post a Comment