Ubalozi wa China nchini Zimbabwe na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) umetangaza kuwa serikali ya China imetoa dola za Marekani milioni 5 kwa Zimbabwe kwa ajili ya msaada wa chakula na ukarabati wa vijiji baada ya mafuriko.
Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Huang Ping amesema, msaada huo wa China unalenga kusaidia vijiji vya Zimbabwe vilivyoathiriwa vibaya na mafuriko kuharakisha kazi za ukarabati na kuanza tena shughuli za kilimo ili kuondoa ukosefu wa chakula.
Mkurugenzi wa WFP nchini Zimbabwe Eddie Rowe amesema, asilimia 40 ya fedha hiyo itatumika katika msaada wa chakula na asilimia 60 itatumika katika ujenzi wa miundo mbinu vijijini
0 Comments:
Post a Comment