Katibu Mkuu CUF Maalim Seif Atuma Bungeni Barua kuwafuta uanacham Wabunge wawili , Spika Job Ndugai ajibu....


August 4, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Maalif Seif Sharif Hamad yenye maelezo ya kuwafuta uanachama wabunge wawili Magdalena Hamis Sakaya na Maftaha Abdallah Nachuma akidai wamekosa sifa ya kuendelea na Ubunge.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa ofisi ya Spika inayo barua ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba yenye kumbukunbu namba CUF/AK/DSM/MKT/05/2017 ya March 22, 2017

 ikiliarifu Bunge kuwa Maalim Seif ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu yatatekelezwa kuanzia tarehe hiyo na Magdalena Sakaya.

0 Comments:

Post a Comment