Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tarime, huku Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko naye akisakwa.
Mhe. Heche amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi hilo kwa madai alizungumza bungeni kuhamasisha wananchi kuzuia shughuli za kampuni ya ACACIA huko Nyamongo, North Mara.
Jeshi hilo pia linadai Mhe. Heche kupitia Mkutano wa hadhara alisema atapeleka hoja bungeni Ili bangi ihalalishwe kuuzwa nje ya nchi, Polisi wanasema kauli hiyo inachochea ulimaji bangi.
Halikadhalika linamsaka Mhe. Matiko ili kumuunganisha katika madai hayo kuwa alizungumza katika Mkutano huo kauli zinazochochea
kilimo cha bangi.
Polisi wamechukua simu za Mhe. alizokuwa nazo, pia wameagiza simu nyingine iliyopo Dar es salaam kwenye matengenezo pia ipelekwe Tarime.

0 Comments:
Post a Comment