Hakuna kitu kilichodondoka ama chombo chochote majini na ndege zilizoripotiwa kuharibika.
Maafisa wa serikali hiyo wamesema kombora hilo lilirushwa kutoka pwani ya magharibi ya Korea Kaskazini hadi kaskazini mashariki mwa Japani kwenye majira ya saa 11 na dakika 58 asubuhi. Kombora hilo linaaminika kutawanyika katika vipande vitatu juu ya Bahari ya Japani na kupita juu ya Rasi ya Erimo kisiwani Hokkaido kati ya saa 12 na dakika 05 hadi saa 12 na dakika 07.
Takribani dakika 14 baadaye kombora hilo liliripotiwa kudondoka katika Bahari ya Pasifiki nje ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Japani ikiwa ni kimolita 1,180 mashariki mwa Rasi ya Erimo.
Maafisa hao wanasema kombora hilo linaweza kuwa ni la masafa ya kati. Wanasema kombora hilo halikuwa katika pembenukta kubwa ambayo inakuwa na pembe kali hivyo kombora hilo huenda lilirushwa katika tao la kawaida.
Wizara ya Ulinzi ya Japani imesema imeweka mtambo wa kudungulia makombora wenye uwezo wa kuzuia makombora katika Bahari ya Japani pamoja na mfumo wa kuzuia makombora wa ardhini wa PAC3. Lakini wizara hiyo imesema mifumo hiyo haikuwashwa.
0 Comments:
Post a Comment