![]() |
| Picha Hii haihusiani na Tukio lolote imewekwa kwa kuzingatia uhalisia wa kinachoelezwa katika habari hii. |
_____________________
Kigali, Julai 22, 2017
Uongozi wa chama cha Afrika Mashariki (EALS), Umoja wa wanasheria wa jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini(SADC LA) na Umoja wa wanasheria wa umajumui wa Afrika (PALU), kwa pamoja tumetizama na kufuatilia maendeleo ya hivi karibuni nchini Tanzania.
Kwa upande mmoja, tumefuatilia suala la hivi karibuni la kukamatwa kwa Rais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), Bw. Tundu Lissu, wakili, wakati akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa EALS Kigali, Rwanda ambako pia vyama dada vilialikwa.
Tunatambua na kukubali haki na zaidi wajibu wa serikali yoyote makini katika kuhakikisha sheria zinafuatwa na raia wote na wotu wengine wanaoishi katika eneo lake; ambayo ni pamoja na haki na wajibu wa kuchunguza jinai zote na kukamata watu wote kwa kufuata taratibu zote za sheria, wanaotuhumiwa kutenda jinai ambazo zimeanishwa na sheria ya nchi au sheria za kimataifa.
Hata hivyo, tumebaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wajumbe wetu, chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), kutoka kwenye taarifa yao ya Julai 21, ijumaa 2017, kuwa utaratibu wa kisheria haukufuatwa wakati wa kumkamata Bw. Tundu Lissu, wakili.
Taarifa iliyotolewa na TLS inasema Bw. Lissu alikamatwa kabla ya taratibu za kiuchunguzi na kimashitaka kukamilika kama inavyotakiwa na katiba na sheria za Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na sheria za kimataifa zinavyotaka, mathalani sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini(SADC), Umoja wa Afrika (AU)
pamoja na zile zinazofahamika kama haki za msingi za binadamu (bills of rights).
Kwakuwa suala hili liko mahakamani, hatutalizungumzia kwasasa isipokuwa kuwakumbusha wahusika wote juu ya umuhimu wa kuheshimu sheria tajwa hususani zinahusu haki za binadamu na ulinzi wa kisheria kwa watu, kama ilivyotokea kwa Bw. Tundu Lissu, wakili.
Tunapanga kufuatilia mwenendo wa usikilizwaji wa kesi ya Bw. Tundu Lissu, wakili, na hatua zingine za kimahama ambazo zimeanza na zitakazofuatia kwajili yake kwa lengo la kulinda haki zake kwa mujibu wa sheria za Tanzania na sheria za kimataifa.
Kwa upande mwingine, tunatambua uwezekano wa matukio yanayoendelea, yanaweza kutafsiriwa kama sehemu moja ya mwendelezo wa hatua na matukio yanayoashiria kudhorotesha mahusiano baina ya serikali na uongozi wa umoja wa taaluma ya sheria nchini Tanzania.
Ni wazi kuwa sio siri kuwa mahusiano yamedhorota tangu matokeo ya uchaguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka kumchagua Bw. Tundu Lissu kuwa Rais wa chama hicho kwajili ya kuongoza kwa muhula wa mwaka mmoja.
Pia tunatambua mwaliko wa hivi karibuni wa waziri wa sheria na katiba wa Tanzania, Mhe. Prof Paramagamba J. A. M. Kabudi, kwa wadau mbalimbali ikiwemo TLS kuwasilisha marekebisho makubwa
ya sheria inayosimamia taaluma ya sheria katika Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Pia tunatambua na kuheshimu haki ya serikali iliyochaguliwa hususani bunge, kusimamia kwa maslahi ya umma masuala mbalimbali ndani ya
mamlaka yake; ikiwemo kusimamia huduma za kitaaluma na tasnia, ikiwemo na taaluma ya sheria.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, usimamizi huo lazima uwe wa faida kwa umma na lazima uheshimu sheria za kimataifa zikiwemo, kanuni za umoja wa mataifa za shughuli za wanasheria za Septemba 1990.
Katika hili, umoja tajwa utawasilisha mambo mbalimbali pamoja na mapendekezo juu ya taaluma ya sheria katika mkutadha wa Afrika, kwa serikali na watu wa Tanzania na kwa nchi zingine zenye hali inayofanana na ya Tanzania.
Kuhusu ushahidi wa wazi wa kudhorota kwa mahusiano kati ya serikali na uongozi wa chama cha taaluma ya sheria katika Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kwa mtizamo wa kufikia malengo, kwa usawa na kwa vitendo, kwa kushirikisha wadau wote, ikiwa ni pamoja na serikali, sekta nyingine za jamii ya Tanzania, Uongozi wa taaluma zote tajwa (EALS, PULA and SADC LA), tutafanya mazungumzo ya kina nchini Tanzania.
Kwasasa tunawasihi Serikali na TLS kuchukuwa hatua za kupunguza taharuki inayoendelea nchini hususani kuhakikisha katiba na sheria za Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na zile za kimataifa mathalani EAC, SADC na AU zote kunaheshimiwa!
____________________________
#Translated by Bob Wangwe

0 Comments:
Post a Comment