Sentensi 2 muhimu za Mbowe baada ya kuachiwa kwa dhamana Mbunge Halima Mdee

"Mdee amesomewa mashtaka ambayo sitaki kuyazungumzia, lakini utamaduni huu mpya unaojengwa ndani ya taifa wa kuziba midomo watu wasiseme hisia zao, utajenga chuki katika jamii. Sisi kama chama cha kupigania haki tunaamini, kila MTU ana haki ya kueleza hisia zake.
“Halima ni mbunge pia ni kiongozi mwandamizi, wakati alivyozungumzia suala la wanafunzi kupata mimba alikuwa akizungumzia kama mwanamke. Hivyo, kama chama kitaendelea kuzungumza bila kujali Polisi na Wakuu wa Wilaya wanatumia sheria ipi. Kama chama kitaendelea kuzungumza bila woga, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli. Tunaamini huku ni kuipotezea muda Serikali pamoja na Mahakama. Time will tell.” – Freeman Mbowe

0 Comments:

Post a Comment