July 05 2017 , Magazeti ya Uturuki na TRT

Hürriyet:Uturuki yatuma barua ya kidiplomasia kwa Ujerumani
Ubalozi wa Uturuki jijini Berlin watoa jibu baada ya uchochezi wa msanii Phlipp Ruch wa Ujerumani .Ubalozi huo umetuma barua ya kidiplomasia kwa wizara ya mambo ya nje .Gari moja liliegeshwa mbele ya majengo ya ofisi ya waziri mkuu Ujerumani na kuwa na mabango yenye picha ya rais Recep Tayyıp ErdoÄŸan ,rais Vladimir Putin na Mfalme Salman bin Abdulaziz.Juu ya picha hizo kuliwa na ujumbe uliosoma "Je ungependa kupata gari hili ? basi ua hawa madikteta ".Polisi wa Ujerumani waliokuwa maeneo hayo walisimama kimya na kuangalia hayo yakiendelea bila kuchukua hatua yoyote .
Habertürk:Hamna kulala Julai 15
Mahir Ünal , naibu mwenyekiti wa chama tawala cha AKP afahamisha kwamba chama hicho kina mipango maalum kwa ajili ya ukumbusho wa jaribio la mapinduzi katika mwaka wake wa kwanza .Aliendelea kusema kuwa baada ya kushinda wahaini wa FETÖ , wananchi wanastahili kusherehekea ushindi huo tarehe 15 na 16 Julai.Rais wa Uturuki atashiriki mikutano ya mkesha katika jiji la Ankara na Istanbul.
Vatan:Uturuki yaendelea kutia fora katika utalii na afya 
Kwa muda wa miaka 5 sasa sekta ya afya nchini Uturuki imeendelea kuimarika jambo ambalo pia linavutia watalii wengi ambao hutembelea Uturuki kwa ajili ya kupata matibabu.Mwaka huu watalii 600,000 wanaotarajiwa kuja Uturuki kwa aji ya kupata matibabu watatumia takriban bilioni 6 sarafu ya Uturuki.Raia kutoka Ujerumani wameonekana sana kupendele Uturuki kwa kupata matibabu.Raia wengine wanaotembelea Uturuki kwa wingi kwa ajili ya afya zao ni kutoka Iraq,Libya,Azerbaijan na Uholani.

0 Comments:

Post a Comment