HIVI PUNDE: Kutoka katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Arusha DC Yamepitishwa maazimio kadha wa kadha !

Halmashauri ya Arusha DC imepitisha maazimio mbalimbali muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya wananchi wa Arumeru.

Moja ya maazimio yaliyoafikoliwa ni pamoja na Uboreshaji wa utoaji Fedha za mikopo kwa ajili ya Vikundi vya Wamama na Vijana.


 Pamoja na Maazimio mengine ni pamoja na suala la miundo mbinu katika barabara za Halmashauri huku wajumbe wakisisitiza kuwa barabara zote ziwekwe Bicon kwa tahadhari kwamba wananchi wajue ukomo wa barabara ili kuepuka usumbufu ambao utajitokeza wakati wa ujenzi wa barabara hizo hapo baadaye.

Huu ni mchoro wa jengo la ukumbi wa mikutano ya Halmashauri ya Arusha DC ambao ni miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa leo.

0 Comments:

Post a Comment