Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mhe. Dkt Vincent Mashinji akiwa na wabunge wawili na viongozi wa Chama wapatao sita leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu mkaza Mkoa wa Ruvuma.
Dkt Vincent Mashinji alikamatwa na Jeshi la Polisi Mbamba-Bay Wilaya ya Nyasa akiwa katika moja wa majukumu yake ya kazi.
Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyasa ilawaachia huru baada ya kukaa ndani kwa Massa 48 kwa amri ya Mkuu wa Mkoa na walitoka kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kwa RPC Mkoa wa Ruvuma 18/7/2017 SAA NNE asubuhi, jambo ambalo walilifanya bila hata kusindikizwa na walitakiwa kupelekwa Mahakamani lakini mwanasheria wa Serikali hakuweza kufika kwa tarehe hiyo jambo ambalo likimpelekea RPC kuwaachia kwa dhamana yao ya awali na kuwataka warudi 19/7/2017 ili kuwapeleka Mahakamani.
Majira ya SAA mbili Dkt Mashinji na viongozi wa Chama walifikisha kwatika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma na kusomewa kesi 173 inayoeleza washitakiwa walitenda kosa na kufanya maandamano pamoja na mkusanyiko usio halali Wilaya ya Nyasa siku ambayo haijulikani wa tarehe haijulikani.
Wakati Kesi haijaanza Jeshi la Polisi walikuwa wakiimarisha ulinzi Mahakamani wakiwa na silaha za moto na kuwataka watu 12 tu ndio waingie kusikiliza kesi hiyo jambo ambalo Wakili wa washatiwa wakiongozwa na Wakili Mbogolo aliiomba mahakama uwape fursa wananchi waliojitokesa kusikiliza kesi kwa kadri Mahakama itakavyoona na Hakimu Kobelo alilitaka Jeshi la Polisi waachia wananchi waingie.
Washatiwa wote wamekana kosa na upande wa Serikali haikuwa na kipingamizi juu ya dhamana yao lakini Hakimu akawataka mawakili waingie chemba ili kujiridhisha na barua za wadhamini.
Wakati zoezi la kukusnaya barua likiendeea Wakili alitoa na kwenda kusikojulikana kwa takribani lisaa limoja na maelezo yalitolewa kuwa amekwenda Mahakama kuu.
Wakati Hakimu ameondoka Jeshi la Polisi liliwatosrosha washtakiwa na kuwapeleka kwenye gereza la Songea Mjini jambo ampalo limeonekana kuwa linaweza kuwa linafanya kiujanja viongozi hao walale gerezani.
Baada la lisaa limoja Hakimu alirudi Mahakamani na mawakili walikwenda kumwambie wadhamini wapo tayari lakini muda huo mwanasheria wa Serikali alikuwa nae kaondoka.
Juhudi za kuwahangaikia viongozi hao watoke zikiendelea kufanywa na viongozi wa Chama wakiongozwa Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi, Katibu wa Kanda ya Nyasa Emanuel Masonga pamoja viongozi wa chama Mkoa wa Songea.
Wakati dhamana zote zimeshakikiwa kwa sasa ni saa nane na dakika arobaini na sita, Hakimu ndio anasubiriwa na muda wa mahakama kufunga kazi ni saa tisa.

0 Comments:
Post a Comment