WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUTUMIA MAMLAKA VIZURI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI),  Mhe. George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia mamlaka yao vibaya ya kuwaweka ndani viongozi,watumishi wa umma na wananchi wengine kwa uonevu kwa kisingizio cha sheria kuwapa mamlaka hayo.
Tokeo la picha la simbachawene
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene
Kauli hiyo ya Waziri Simbachawene ameitoa leo bungeni  ikiwa ni baada ya wabunge kuhoji uwepo wa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kutoa amri ya kukamatwa kwa watu bila sababu ya msingi hivyo ni hatua gani serikali inachukua dhidi yao kukomesha tabia hiyo.
Ni kweli sheria hii ya mikoa inatoa mamlaka ya kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuweza kumkamata mtu katika mazingira ambayo wanaamini kwamba mtu huyo ama anatenda kosa la jinai ama kwa ufahamu wao ametenda kosa la jinai ama anatenda kitendo chochote kinachovunja amani na utulivu ama anaona mtu huyo anatarajia kutenda au kuhatarisha amani hiyo ndiyo tafsiri ya sheria waliyopewa.”amesema waziri Simbachawene.
Akiendelea kusisitiza amesema licha ya sheria kuwapa viongozi hao mamlaka hayo wanapaswa kuwa makini wanapoitumia sheria inavyotamka kwa kuzingatia mipaka yao ya kazi katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa.
Mtu yeyote anayo haki ya kuomba mtu mwingine ambaye anaweza kutenda kosa la jinai dhidi ya mtu fulani au watu fulani kuomba  wakamatwe kwa hiyo haki hii sio tuu wamepewa hawa peke yao…. isipokuwa tuu cha msingi ni pale tuu ambapo inapaswa kutumika kwa kuzingatia sheria mtu huyo awe anamatarajio ya kupelekwa mahakani immediately baada ya kukamatwa na baada ya muda ule kupita asikamatwe mtu kwa ajili ya ku’ Show Off , asikamatwe kwa ajili ya kuonesha kwamba wewe una madaraka lazima akamatwe mtu huyo kama kweli kitendo chake kinahatarisha amani na utulivu na hapa ndipo nataka nisisitize kwamba wakuu wetu wa mikoa na wilaya kwa kutumia sheria hii wawe makini kwa kutumia sheria hii kama inavyotaka.“amesema Waziri Simbachawene.
Sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 1997 sura ya 97 inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kumweka ndani mtu ye yote kwa muda wa saa 48 ikiwa itathibitika kuna hatari ya uvunjifu wa amani na usalama au mtu huyo ametenda kosa la jinai.

0 Comments:

Post a Comment