Baada ya kujiuzulu kwa Diwani huyo haya ni maneno mazito aliyaongea Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini Mh. Amani Golugwa
"Wanaotaka kuondoka waondoke sasa, kazi tuliyo nayo ni kubwa mbele yetu. Kamwe hatutahesabu hasara yoyote kuondoka. Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na yenye kuhitaji kujitoa kwa dhati. WanaCHADEMA msisikitike, wamechelewa kuondoka na msione kuwa wanatushtukiza, hapana wao ndio wamekaa kwa mateso sana na sasa hawana budi kuondoka maana hawakuwa Wa kwetu. " Yai likishakuwa viza halina thamani tena ya kukaa kwenye trei la mayai mazuri".
Wataondoka kadhaa, tusipaniki tuwaache waondoke, tulijua baadhi yao wataondoka na tunajua baadhi yao wapo njiani kuondoka, tuwaache waondoke kwa kujichinja wenyewe. Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa na inahitaji waliojitoa hasa na wenye mapenzi mema na nchi hii na sio unafiki.
Hila yao kwa kupindi walicho kaa nasi na dhambi yao ya maneno ya uongo wakati wa kuondoka kwao watailipa tu
Amani Golugwa-Katibu wa Kanda ya kaskazini.
0 Comments:
Post a Comment