TAKUKURU Imewakataza Viongozi Wa TFF kwenda Usahili

TAKUKURU imekataa kuwaruhusu viongozi wa TFF wanaoshikiliwa kwenda ktk usahili wa wagombea unaoanza leo. Viongozi hao ni wagombea. Soma https://goo.gl/fvY2Xv
Kutoka Kushoto ni Mwesigwa Celestine katibu Mkuu Tff,  Jamal Malinzi Rais wa TFF, Geofrey Nyange Kaburu Makamu wa Rais Simba na Evance Aveva Rais wa Simba... Wote wamepandishwa kizimbani muda huu
Kutoka KISUTU

Malinzi, Mwesigwa na Nsiana wamesomewa mashtaka 28...

Kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa EXCOM imeridhia kubadilishwa kwa Signatories wa Bank hii inamhusu Malinzi na Mwesigwa pia,

Kufoji risiti za kuwa Malinzi anaidai TFF (risiti zipo zaidi 20 zinazodaiwa kufojiwa) hii inamhusu Malinzi pekee

Na Mwisho ni shtaka la kutakatisha fedha dola za kimarekani 375418 hii inamhusu Malinzi, Mwesigwa na Nsian

Taarifa hii fupi imeandaliwa na   mwandishi wa Star TV Ahmed Ally,ambaye yupo Mahakama ya Kisutu.

0 Comments:

Post a Comment