UPDATES: WAZIRI MKUU WA UINGEREZA KUUNDA SERIKALI MPYA

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anatafuta kuunda serikali mpya licha ya chama chake cha Conservative kupoteza kuongoza kwa wingi wa viti bungeni katika uchaguzi mkuu wa juzi Alhamisi.

Huku zoezi la kuhesabu kura likielekea kukamilika, matokeo ya viti 649 kati ya 650 tayari yameshajulikana. Conservative kilipata viti 318, ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na jumla ya viti 330 kilichopata kwenye uchaguzi uliotangulia. Chama hicho kililenga kujinyakulia viti 326 ili kiongoze kwa jumla ya wingi wa viti bungeni. Chama cha upinzani cha Labour kimepata viti 261. Scottish National Party kilipata viti 35 na Liberal Democrats viti 12.

Waziri Mkuu May ataelezea nia yake ya kutaka kubaki mamlakani. Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu huyo alifikia maafikiano na chama cha Northern Ireland ya kumuunga mkono.

Ukosoaji dhidi yake unazidi kuongezeka hata ndani ya serikali yake kwa kushindwa kupata wingi wa viti bungeni kwenye uchaguzi huo mkuu wa mapema. Matokeo hayo pia huenda yakawa na athari kubwa kwenye majadiliano ya Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

0 Comments:

Post a Comment