Msemaji wa rais İbrahim Kalın aikosoa jumuiya ya kimataifa kwa kuendelea kupuuza matendo ya kigaidi yanayotendewa Uturuki na PKK
Dunia inaendelea kupuuza mauaji yanayoendelezwa na kundi la kigaidi la PKK
Msemaji na mshauri wa rais wa Uturuki İbrahim Kalın akosoa vikali dunia na vyombo vya kigeni vya habari kwa kupuuza matukio ya hivi karibuni ya PKK dhidi ya raia .
Mnamo Juni 9 PKK walijaribu kushambulia gari lililokuwa limebeba mkuu wa manispaa ya Batman Veysi Işık lakini aliweza kuokolewa.
Baadaye tena gari lililokuwa na vilipuzi liligunduliwa karibu na Gendarme na kuweza kuharibiwa .
Msemaji wa rais İbrahim hata hivyo amekosoa vikali vyombo vya habari vya kigeni kwa kupuuza mauaji ya askari mmoja na mwalimu wa miaka 22 wa kike yaliyotekelezwa na PKK kanda ya kusini Mashariki mwa Uturuki wiki iliyopita .
Gari lililokuwa limetegeshwa maeneo ya gendarme lilipelekea askari wawili kujeruhiwa ambapo baada mmoja ya askari kwa sababu ya majeraha mabaya alifariki .
Kwa mara nyingine tena mataifa ya magharibi yamepuuza matukio hayo ya kigaidi yanayoendelezwa Uturuki.Hamna taarifa maalum katika vyombo vya habari vya kimataifa zilizangazia matukio hayo na PKK .Hakuna kiongozi wa kimataifa aliyekemea wala hata kulaani mashambulizi hayo.Cha kushangaza ni kuwa ni hao hao viongozi wa kimataifa ndio hujidai na kutoa wito kwa kuwa na muungano dhidi ya makundi ya kigaidi na pia kutaka kufanya mijadala ya mikakati ya kupambana na ugaidi.
Msemaji wa rais Kalın alishiria kuwa vitendo kama hivyo na mataifa ya duniani yanaonyesha kuwa sasa ni kipindi cha unafiki wa hali ya juu na pia kipindi cha ugaidi uliopita kiasi duniani.
Tangu mwaka 1984 PKK wamekuwa wakitekeleza mashambulizi yanayolenga walimu na hadi kufikia sasa takriban walimu 150 wamepoteza maisha yao.Hii ni mpango wa PKK kudhoofisha kiwango cha elimu katika jamii ya wakurdi huku maelfu ya watoto katika jamii hiyo wakinyimwa haki yao ya kupata elimu.Walimu wengi nchini Uturuki hushindwa kujisajilisha nafasi za kazi katika kanda ya Kusini Mashariki kwa kuhofia maisha yao.
Mnamo Septemba mwaka 1994 magaidi wa PKK walivamia shule moja maeneo ya Tünceli na kuwateka nyara walimu 6 kutoka shule za umma.Kisha wakawapeleka uwanjani na kuhakikisha kuwa raia wanatazama matendo yao ya kinyama dhidi ya raia kwa kuwaua walimu hao mbele ya halaiki ya watu.
Baada ya miezi mine tena PKK waliwaua walimu wengine wanne katika shule moja Tekman ,Erzurum .
Kalin amefahamisha kwamba baada ya kila shambulizi Marekani na Ulaya ,nchi zilizoshambuliwa huchukua hatua ya kwanza kwa kuongeza na kudhibiti usalama kwa ajili ya raia wake .Aliendelea kusema kwa ni haki yao kuchukua hatua kama izo .Lakini cha kushangaza ni kwamba Uturuki ikichukua hatua kama hizo tena huwa kuna matendo mengi ya kinafiki dhidi yake na mataifa mengine .Ugaidi sasa umekuwa changamoto kubwa zaidi duniani na pia tishio kuu ulimwenguni.
Kundi la kigaidi la PKK liliorodheshwa kama kundi la kigaidi mnamo mwaka 2015 na Uturuki na EU baada ya kuanzisha mashambulizi ya kigaidi dhidi ya raia.Tangu mwaka huo PKK imetekeleza mauaji ya watu 1,200 miongoni mwao watoto na wanawake .
Serikali ya Uturuki inatambua makundi ya PYD na YPG pia kuwa matawi ya kundi la PKK yaliyopo nchini Syria .
Lakini Marekani imechukua hatua ya kuhusisha PYD/YPG katika kupambana dhidi ya DAESH katka operesheni ya hivi karibuni ya Raqqa.
0 Comments:
Post a Comment