Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro Picha ya V.O.A TV |
Amesema kitendo cha mkuu wa mkoa kumuweka chini ya ulinzi Yeye (Meya), Viongozi wa dini pamoja na Waandishi wa habari ni kosa kubwa na kwamba anastahili amtake radhi vinginivyo atamfikisha mahakamani ndani ya siku saba (7) asipofanya hivyo.
Nimekuwekea Full video kutoka V.O.A TV bonyeza litufe cha paly
Vilevile Mstahiki Meya Anasema amegundua Mkuu wa mkoa Bw. Gambo anamatatizo ya muda mrefu "Nimegundua kuwa Mh. Gambo anamatatizo ya muda mrefu. Nimeongea na Mwenyekiti wa halmashauri ya Korogwe Mh. Kalage kwamba aliwahi kuingia mgogoro na Mrisho Gambo akiwa DC wa Korogwe na mpaka ikafikia hatua akafukuzwa kwenye uwenyekiti akarudishwa na waziri, Mh. Mkuu wa mkoa amekuwa na vurugu kubwa Korogwe na hapa nina hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa tarehe 09/09 alikuwa na tabia ya kuweka watu ndani alimuweka ndani huyu dada anaitwa Najum Teka ambaye alikuwa mwanasheria wa Korogwe na alimtukana matusi ya Nguoni" Alisema Meya Kalisti Lazaro.
Je! RC Gambo aliwahi Kuhukumiwa?
Kama kawaida jukumu langu ni kukuhakikishia kuwa haupitwi na chochote sasa nimekusogezea na facts juu ya jambo hili la mkuu wa mkoa kuwahi kuhukumiwa kwa kosa la kutumia mamlaka ya umma ndivyo sivyo.Hapa nimekuwekea Screenshot ya nakala ya hukumu aliyowahi kuhukumiwa nayo mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. Hukumu ambayo iliendeshwa na jaji wa mahakama kuu ya Tanga Jaji Janja , hukumu hiyo imetokana na kosa la udhalilishaji dhidi ya wanawake kwa kumtukana Aliyekuwa mwanasheria wa halmashauri ya Korogwe Tanga.
katika hukumu hiyo inaonekana matusi aliyoyatoa Mrisho Gambo kwa dada huyo aliyefahamika kwa jina la Najum Teka ambaye kwa mujibu wa hukumu hiyo alikuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe.
Hukumu hiyo ilifikia kikomo kwa mahakama chini ya jaji Amuru Hussein kuamuliwa kuwa Mrisho Gambo amlipe fidhia kwa udhalilishaji wa wanawake. " Mpaka leo hakulipa kama dada wa watu kama jaji alivyoamuru , Hauwezi kuhukumiwa na jaiji Tanga halafu unaenda kwa jaji mwingine kula kiapo , hii ni kuidanganya mahakama , taasisi za serikali na kumdanganya Rais"
kwa mujibu wa hukumu hiyo Mrisho Gambo alitakiwa kulipa millioni 20 kama"general damages"na millioni tano kama gharama za kesi na Asilimia 7 ya riba tangu kesi ilipoanza.
Swali la Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha kwa Rais JPM
"hii kesi imeendeshwa tangu tare 25/05/2015 kwa maana hiyo ni kwamba wakati Rais anafanya uteuzi wa wakuu wa wilaya 2016 baada ya ushindi wake haikufanyika veting huyu ana hukumu ya uzalilishaji" Swali
"
Nataka nimuuulize Rais ana hii hukumu ya jaji?"
Aidha Mh. Meya aliongeza kuwa hana tatizo binafsi na mkuu wa mkoa Bw. Mrisho Gambo " Sina tatizo binafisina mkuu wa mkoa nina tatizo na matendo yake , tabia yake"
Meya anasema Mh. mkuu wa mkoa alitakiwa kumsifu yeye kwa kutokana na halmashauri yake kuwa halmshauri bora nchini ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ambapo tayari imefanikiwa katika utekelezaji wa bajeti kwa asilimia 96 na hadi kufikia mwezi juni 30 bajeti itakuwa imetekelezwa kwa asilimia zaidi ya 100 "Halmashauri yangu ni halmashauri bora kwa kukusanya mapato" Bw. Kalisti
"Msichana huyo amasomeshwa na na wazazi wake kwa gharama leo anamtukana matusi ya nguoni"
Mambo 5 aliyopendekeza Mstahiki Meya kwa RC Gambo
1. "Alipe gharama zote alizohukumiwa nazo kwnye hii kesi kama hukumu inavyoelekeza .
2. " Amuombe Radhi Najum Teka kwa Matusi aliyomtukana na aombe radhi wanawake wa Tanzania na wanawake wa arusha
3. Awaombe radhi Watanzania kwa kwamba yeye amekuwa tabia ya kudhalilisha"
4. "Aniombe radhi mimi kwa kuniweka ndani kwa kosa ambalo mpaka leo silijui , Meya mwenye heshima kwa sababu tu ya kupeleka rambi rambi, amemuweka Padri wangu ndani, Kiongozi wa Bakwata Olasiti, amewaweka waandishi wa habari Aombe radhi kwa kitendo alichoamrisha kwa jambo ambalo si ubinadamu"
5. "Atakafari kama bado anastahili kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa sababu anawatumikia wananchi ambao hana heshima nao huwezi kumheshimu Mbunge , Madiwani , viongozi wa dini wala huwezi kuheshimu waandishi wa habari"
Asipotekeleza
1. Asipomuombaradhi yeye (Meya)
Meya Kalisti Lazaro amesema Mkuu wa mkoa asipoomba radhi kwa kitendo cha kumkamata yeye , Viongozi wa dini na Waandishi wa habari atawachukua wote aliokamatwa nao na kumfikisha mahakamani Mkuu wa mkoa Mh. Gambo kama Gambo"nitakutana naye mahakamani at his own capacity kama Mrisho Gambo kwa sababu mamlaka aliyotumia siyo ya RC. kama alivyoshtakiwa na huyo dada akashindwa"
2. Asipomuomba radhi na kumlipa huyo dada (Najum Teka)
Video Ipo hapa Bonyeza Play
Kuhusu endapo mkuu wa mkoa hatotekeleza hilo meya anasema atakwenda maadili kwa kufuata taratibu za kisheria kutazama file za Gambo kuona mali alizonazo ili kuziuza na kulipwa madai ya fidhia ya Najum Teka Mwanasheria wa Korogwe anayedaiwa kudhalilishwa na Mrisho Gambo kwa kutukanwa matusi ya nguoni ambapo mahakama iliamuru mshtakiwa amlipe mshtaki kwakuwa alishindwa hiyo kesi"
"Tunajua mali zake,ameambiwa alipe gharana hizi hataki kulipa,nitaenda maadili nitakagua fomu yake aliyojaza mali alizoorodhesha zikamatwe na kulipwa huyo dada kama fidia ya gharama anazomdai"
3. Asipowaomba radhi wanawake
"Nitaomba wanawake wa Arusha waandamane kulaani kutukanwa kwa wanawake waliosoma na wenye degree tanzania"
katika kumalizia Mh. Meya amezungumzia kuhusu wafanya biashara wa jiji la Arusha ambapo alimtaka mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo aweke wazi utaratibu ili iwe rahisi wakati wa kuwatumikia wananchi. "Mkuu wa mkoa alikusanya hela kutoka kwa wafanya biashara za pikipiki kwa ajili ya vijana wa Arusha kimaadili sisi viongozi unapofanya jambo lazima ufuate utaratibu wa kiserikali nataka nimwambie mkuu wa mkoa aweke wazi, alitumia utaratibu upi wa kununua hizo pikipiki" Alisema Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro.
Kuhusu Maendeleo ya jiji la Arusha
"
Halmashauri yangu ni halmashauri bora katika ukusnyaji mapato nilifikiri RC angekuwa mtu wakunisifu"
katika kumalizia Mh. Meya amezungumzia kuhusu wafanya biashara wa jiji la Arusha ambapo alimtaka mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo aweke wazi utaratibu ili iwe rahisi wakati wa kuwatumikia wananchi. "Mkuu wa mkoa alikusanya hela kutoka kwa wafanya biashara za pikipiki kwa ajili ya vijana wa Arusha kimaadili sisi viongozi unapofanya jambo lazima ufuate utaratibu wa kiserikali nataka nimwambie mkuu wa mkoa aweke wazi, alitumia utaratibu upi wa kununua hizo pikipiki" Alisema Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro.
0 Comments:
Post a Comment