MAGAZETI: Vichwa vya Habari vikuu Magazeti ya Uturuki leo, Kikundi cha kigaidi cha FETO ilikuwa gumzo pia

Yeni Åžafak:Maadui wa Uhuru
Ujerumani inaendelea kuchukua hatua ambazo zinakiuka uhuru na haki za kibinadamu.Berlin inamtaka rais Recep Tayyıp ErdoÄŸan kutoambatana na walinzi wake wakati atakapohudhuria mkutano wa G20 nchini Ujerumani.Ankara imekosoa vikali hatua hii .Msemaji na mshauri wa rais İbrahim Kalın amesema kwamba hawatokubali hatua na nia mbaya za baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani.Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki naye pia amafahamisha kwamba  hesabu za ndani za Ujerumani zinakemewa vikali huku waziri wa EU nchini Uturuki akifahamisha kwamba hatua za Ujermani hazionyeshi ulinzi wa uhuru bali zinaonyesha ukosefu wa heshima kwa uhuru.
Star:Merkel azuia hatua ya kurudishwa kwa wahaini wa FETÖ
Ugiriki ilikuwa imechukua hatua ya kuwarudisha wahaini wa FETÖ ambao walishiriki katika jaribio la Mapinduzi Uturuki.Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibu wabainisha kwamba kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezuia Ugiriki kuchukua hatua hiyo.Haya yamaebainshwa na mbunge wa Kituruki nchini Ujerumai katika chama cha Syriza Mustafa Mustafa.Mustafa alifahamisha kwamba Athens ilibadilisha mawazonya kuwarudisha wafuasi wa FETÖ baada ya Berlin kutofurahishwa na hatua hiyo.
Habertürk: Kongamano la mwisho kwa ajili ya Ugiriki
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu ametoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu Kongamano la Cyprus linaloendelea Crons-Montana nchini Uswizi.Waziri Çavuşoğlu alisema kuwa kongamano hilo linanuiwa kuwa la mwisho kwa ajili ya mzozo wa Cyprus."Iwapo kutakuwa na suluhu sharti kuwe nalo kipindi hiki na enedapo suluhisho halitapatikana basi ina maana kwamba halitopatikana tena ".

0 Comments:

Post a Comment