Machache yaliyochapishwa katika Magazeti ya Uturuki Leo..

Muhtasari wa habari za Magazeti Uturuki
Gazeti la Yeni Åžafak:Unafiki wa nchi ya Ujerumani 
Nchi ya Ujerumani inatambulika kwa kuunga mkono makundi karibu  yote ya kigaidi imeanzisha sakata mpya .Ni wazi kwa Ujerumani iliwakaribisha na hata kutoa msaada wa kifedha kwa makundi ya kigaidi kama FETÖ na PKK 
.Ujerumani imeonekana kutofurahishwa na jinsi walinzi wa ErdoÄŸan walipowashambulia wafuasi wa PKK nje ya ikulu ya White House kipindi rais ErdoÄŸan alipotekeleza ziara ya Marekani mwezi Mei.Berlin imefahamisha kwamba walinzi wa rais ErdoÄŸan hawataambatana na rais huyo katika mkutano wa G20 utakaofanyika tarehe 7 na 8 mwezi Julai.Ujerumani imefahamisha kwamba ikiwa walinzi hao wataenda ,watakamatwa na kupelekwa Marekani washtakiwe.

Gazeti la  Habertürk: Elfu 20 ya watalii wataambana na wafanya likizo kutembelea Uturuki 
Kufuatia wito wa rais Recep Tayyıp ErdoÄŸan kwa raia wa Uturuki waishio nje ya kuwa kuwaleta majirani zao kipindi wanapokwenda Uturuki kwa likizo,inaonekana kampeni hiyo inafanya kazi mno.Idadi kamili ya watalii watakaotembelea Uturuki wakiwa na watakaokwenda Uturuki kwa ajili ya likizo imebainika .Mkurugenzi wa kampuni za kuleta watalii Kadir UÄŸur kutoka Uholanzi,Ujerumani,Austria na Uswizi afahamisha kwamba asilimia 38 ya watalii itakwenda Uturuki.Kati ya watalii 120,000 watakaotembelea Uturuki 20,000 watakwenda Uturuki kupitia kampeni ya 'Njoo na jirani yako'.
na Gazeti la Hürriyet: Bingwa wa Dunia
Katika mashindano ya Taekwondo nchini Korea Kusini ,mwanamke Nur Tatar Askari amejishindia medali ya dhahabu katika mashindano ya wanawake ya uzito wa kilo 67 .Mwanamchezo huyo wa Kike wa kitaifa kutoka Uturuki alimshinda mchezaji mwenzake kutoka Marekani Paige McPherson 6 kwa 4 katika roundi ya mwisho ya mashindano hayo .Mwanariadha huyo atarajiwa kushiriki olimpiki za mwaka 2020 Tokyo.

0 Comments:

Post a Comment