HABARI: Serikali imepiga Marufuku usafirishaji wa Mahindi nje

Image result for Kassim MajaliwaSerikali imeweka marufuku ya kuuza mahindi nje ya nchi ikiwa ni hatua ya kufanya wananchi wawe na chakula cha kutosha ili kuepusha tatizo la njaa hapo baadaye.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameema kwa yeyote atakayebainika kusafirisha nje ya nchi chakula hicho kitakamatwa na kupelekwa katika hifadhi ya taifa ya chakula.
''Kuanzia leo, yeyote atakayepatikana anasafrisha chakula kutoka nchini kuelekea nchi jirani , chakula hicho kitachukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya kitaifa na lori lililotumika kusafrisha mzigo huo litakabidhiwa maafisa wa polisi'', alisema.
''Serikali haitaruhusu uuzaji huo hususan wa unga wa mahindi kwa sababu utasaidia viwanda vya kitaifa''.

0 Comments:

Post a Comment