IRAN: Watu zaidi ya 56 Million wanatarajiwa kupiga kura nchini humo, kuna uhakika wa zaidi ya 72% ya wapiga kura kuhudhuria

Raia kuanzia miaka 15- wakitekeleza haki yao yakupiga kura nchini Iran.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Abdolreza Rahmani-Fazli, alisema hayo jana usiku katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na Kanali ya Pili ya Televisheni ya Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB na kuongeza kwamba, watu milioni 56 na laki nne na elfu 10 na 234 wametimiza masharti ya kupiga kura nchini Iran. Ameongeza kuwa, karibu maafisa milioni moja na laki tano wanaendesha na kusimamia uchaguzi huo.

0 Comments:

Post a Comment