BURUDANI: Roma Mkatoliki adai hana kadi ya Chama chochote

Related image
Roma Mkatoliki
Mwanamuziki Roma Mkatoliki Asema hafungamani na upande wowote kisiasa 

“Naendelea vizuri, baadhi ya vidonda vimeanza kukauka. Mimi sifungamani na upande wowote, sina kadi ya chama chochote. Kwa sababu nikichukua kadi ya chama chako nakuwa familia yako, hata hivyo mimi ni Mkristo ‘Mkatoliki’, kwa hiyo katika hali ngumu huwa nasali kumuomba Mungu.

Apinga vikali kauli ya Ally Kessy mbunge wa Nkasi kuwa alimuimba Rais JPM , 

“Tena alitaja kabisa jina langu. Lakini ameongea vile kwa sababu yeye ana mahali pa kusemea. Je, mimi nitasemea wapi? Hayo maneno bora angeongea Rais wa Manzese Madee ningejua swahiba wangu ananitania.

Roma adai kwa sasa pia kikazi wamekwama

“Mimi ni msanii, mimi ni mfanyabishara. Hivyo lazima kazi ziendelee. Ndio maana hata sasa nimeona nitoke kuhangaika ili tuendelee. Kama tunaweza kusaidiwa, tunaomba mtu yeyote aweze kuona jambo la studio kwa jicho tofauti.” Roma Mkatoliki.


0 Comments:

Post a Comment