Habari: Meli za Kivita za marekani zafika Korea

USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia
Sab-Marine ya USS Michigan Inayotumia nguvu za nyuklia

Meli ya jeshi la Marekani imewasili katika pwani ya Korea Kusini huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia.


Meli hiyo kwa jina USS Michigan, ambayo ina uwezo wa kushambulia kwa makombora, inatarajiwa kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo, zikiongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege za kivita ya Carl Vinson.
Korea Kaskazini inaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa jeshi lake Jumanne.
Miaka ya nyuma, imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa kuzindua makombora na silaha nyingine.
Hali ya wasiwasi imetanda kwamba huenda Korea Kaskazini ikarusha Kombora au Nyukilia!

0 Comments:

Post a Comment