MWENYEKITI wa Serikali ya kijiji Msitu wa Mbogo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ernest Mkilanya amehukumiwa kwenda jela miaka 15 pamoja na wenzake wanne baada ya kupatikana na hatia ya kufanya kosa la unyan'ganyi wa sh 785,000 kwa kutumia nguvu.
Uamuzi huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na hakimu ya Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai
iliyopo Wilayani Arumeru, David Mwita ambaye alisema kuwa mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na pande zote.
Wengine waliotiwa hatiani ni pamoja na mdogo wa Mwenyekiti hiyo, Simon Mkilanya na Juma Maulidi ambao ndiyo walikuwepo mahakamani hapo wakati uamuzi huo ukitolewa huku wengine Edwin Deo na Julius John wakitafutwa ili nao wakatumikie adhabu hiyo gerezani Kisongo.
Hakimu Mwita alisema kuwa mahakama hiyo imewaona Mkilanya na wenzake wanne kuwa wanahatia na wanastahili kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka 15 jela baada ya pande zote kuwasilisha ushahidi na utetezi juu ya shauri hilo la unyang'anyi wa kutumia nguvu lililopo chini ya kifungu cha sheria namba 286 cha kanuni ya adhabu kilichopitiwa upya mwaka 2002 .
Alisema kuwa mshtakiwa Mkilanya na wenzake walitenda kosa hilo Septemba 11, 2014 eneo la Msitu wa Mbogo ambapo yeye na wenzake walimkamata na kumfunga mikono malalamikaji
kwenye shauri hilo, Petro Damas na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Hakimu Mwita alisema kuwa kwa mujibu wa sheria kifungu namba 286 mahakama hiyo ya mwanzo inamamlaka ya kutoa hukumu hiyo kwani kosa hilo ni miongoni mwa
mwongozo wa sheria ya mahakama sura ya 90 kifungu namba 5 (a) ( i)
kinachosema kuwa mtu yoyote atakayepatikana na hatia katika kosa hilo
kifungo chake si chini ya miaka 15.
Alisema mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo kwa mujibu wa sheria na
kanuni zilizopo hivyo washtakiwa hao watatu watatumikia kifungo hicho
huku washtakiwa wengine wawili ambao ni Deo na John wataendelea
kutafutwa na watakapopatikana watakamatwa na kufukishwa mahakamani
hapo kisha mahakama itatoa nafasi ya kuwasikiliza kisha kutoa hukumu
kwa mujibu wa sheria
AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAWATOA HOFU WATEJA WAKE WA KARIAKOO
-
Akiba Commercial Bank Plc imeendelea kujitoa si tu kuhudumia wateja wake
bali pia kushiriki katika juhudi za kijamii wakati wa dharura na majanga,
ikiwa ...
10 hours ago
0 Comments:
Post a Comment