NANYARO AELEZA KWA NINI ACHAGULIWE KUONGOZA BAVICHA

Namshukuru sana Mwenyenzi Mungu kwa wingi wa neema na rehema zake.Nitumie
fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati kabisa viongozi wa BAVICHA Taifa wanaomaliza
muda wao(John Heche Mwenyekiti na Deo Munish Katibu Mkuu)nawapongeza kwa kazi
kubwa na nzuri waliyoifanya na leo BAVICHA ni taasisi kubwa na imara.Pia nawapongeza wote
waliochaguliwa kuongoza BAVICHA kuanzia ngazi za misingi,matawi,kata,Wilaya na Mikoa.
Mimi Ephata Nanyaro nimezaliwa tarehe 27.11.1984,nina mke mmoja na watoto wawili.Elimu yangu ni shahada ya kwanza
UZOEFU WA KIUONGOZI NDANI YA CHAMA
-Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Arusha(2009-2014)
-Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arushamjini(2011-2014)
-Diwani wa kata ya Levolosi Arusha Mjini(2010-2015)
_Mmoja wa waanzilishi wa VIPATU taasisi yavijana ambayo imeinua vijana wengi Kiuchumi mkoa wa Arusha
KWA NINI NAFAA KUWA MWENYEKITI
1.Uwezo wa kiuongozi
Nimekiongoza chama wilaya ya Arusha mjinikwa mafanikio makubwa sana,katika kipindi cha uongozi wangu tulifanikiwa kushindachaguzi zote ndogo,na kata ya Sombetini na Daraja mbili ambazo awali zilikuwa ccm tukazirejesha CHADEMA.Nimewatumikia wanawanchi wangu wa Levolosi kwa uaminifu
na uwezo mkubwa,ambapo tumeweza kutekeleza ahadi zetu kwa 80% hadi sasa.
2. Ubunifu
Tumebuni miradi mbalimbali ya BAVICHA Mkoa wa Arusha,yenye malengo ya (a)Kuboresha na
kuinua maisha ya vijana kiuchumi(b) Kukifanya chama kuwa relevant kwa wananchi
wengi.Chini ya mpango huu tulianzisha VIPATU (Vijana pamoja tunaweza)

3.Oganizesheni imara ya BAVICHA Kwa kuwa malengo makuu ya chama ni kuchukua DOLA,na BAVICHA ina jukumu kubwa la Kuhakikisha malengo makuu yachama yanafikiwa.Hivyo tunahitaji kujenga
oganaizesheni imara ya BAVICHA kutoka chini hadi juu.BAVICHA itakayokuwa mhimili mkuu
wa CHAMA katika kufikia malengo, hili tutalijenga katika misingi ya Uadilifu,Uwajiikaji,Uwazi,Utu na Ujasi ri mkubwa sana  Kwa heshima sana naomba KURA kwa vijanawenzangu,wajumbe wote wa mkutano mkuu
wa BAVICHA,na wasio wajumbe ninawaomba sana mniunge mkono katika kuwatumikia
vijana .Hakika ukinichagua hutoijutia kurayako.

CHAGUA NANYARO BAVICHA 2014-2019
Kuhakikisha BAVICHA inafanikisha malengo ya CHADEMA.Kuhakikisha dira kuu ya BAVICHA inafikiwa
yaani vijana kuwa nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya Taifakwa ujumla
.Kuwezesha sera sahihi,uongozi bora na kujenga oganizesheni dhabiti ya vijana kwa maendeleo endelevu
.Mafunzo ya maswala ya kijamii(afya,uchumi,demokrasia,na uongozi)
.Chemichemi ya uongozi
"And there comes A time when one must take a position that is
neither safe, nor politic, nor popular but he/she must do it because CONSCIENCE tells him
it is RIGHT" Ephata Nanyaro BAVICHA 2014-2019