Uhalifu mpya waibuka Arusha wanawake wanaoendesha magari wapigwa risasi


 

JIJI la Arusha limekumbwa na taharuki baada ya kuibuka kwa  kwa matukio ya wanawake wanaoendesha magari kuvamiwa na kupigwa risasi na watu wasiofahamika ambao hutoweka bila kuchukua chochote ambapo mpaka sasa jumla ya wanawake watatu wamekumbwa na kadhia hiyo huku mmoja akifariki.

Aidha, Jeshi la polisi linaangalia uwezekano wa kufunga kamera ili kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayolikumba jiji hili ambapo kwa sasa wanaendelea na majadiliano na wadau mbalimbali ili kufanikisha hilo.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatusi Sabas, jana alithibitisha kutokea kwa matukio hayo aliyosema kuwa mawili yametokea eneo la Sakina kwa Iddi na moja lilitokea eneo la Mbauda ingawa hakuwa tayari kutaja jina la mwanamke huyo aliyedai kuwa alipigwa risasi lakini haikumpata.


Alisema kuwa mpaka sasa hawajajua sababu ya matukio hayo ambayo walengwa wakuu wamekuwa ni wanawake wanaoendesha magari hivyo akaomba jamii kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa watu hao.

 

 Sabas alisema kuwa aliyefariki ni  Shamim Rashid Yulu, (30) ambaye  alipigwa risasi shingoni juzi majira ya saa 3.30 usiku wakati akikaribia kufika kwenye geti la nyumba yake maeneo ya Sakina kwa Iddi wakati akiendesha gari yake yenye namba za usajili T 566 BYA  aina ya Toyota Ipsun.

 

"Akiwa peke yake alipokaribia geti la nyumbani kwake ghafla aliona pikipiki ambayo namba zake za usajili zilikuwa zimetolewa na ikiwa na vijana wawili ambao walimsimamisha marehemu na kufyatua risasi moja hewani.

"Kitendo kilichomfanya marehemu kuongeza kasi ya gari lakini majambazi hao walifanikiwa kumjeruhi na kumpora simu mbili aina ya nokia na Samsung," alisema Sabas.

 

Alisema kuwa marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Selian.

 

Kamanda Sabasi alisema kuwa tukio lingine  lililotokea mwanzoni mwa wiki eneo hilohilo la kwa Iddi ambapo majira ya saa 1:00 usiku , Florah Porokwa alipigwa risasi kifuani wakati akiendesha gari lake aina ya Toyota Harrier.

 

Alisema kuwa wakati mwanamke huyo akielekea nyumbani kwake alivamiwa na watu wawili waliokuwa kwenye bodaboda na kumpiga risasi lakini mwanamke huyo alijitahidi kuendesha gari hilo mpaka karibu na nyumbani ambapo alipoteza fahamu kutokana na kutokwa na damu nyingi kisha majirani walimsaidia kumwahisha hospitali.

 

Mume wa Florah, Edward Porokwa ambaye ni mkurugenzi wa Shirika liliso la kiserikali la kutetea haki za wafugaji, (Pingo's),  aliiambia Tanzania Daima jana kuwa mke wake anaendelea vizuri ingawa bado amelazwa kwenye hospitali ya Selian anapopatiwa matibabu.

 

KATIKA tukio lingine Jeshi la polisi, linawashikilia watu wanne kuhusiana na matukio ya kigaidi ambapo mmoja kati yao, Adam Pakasi, (34), amekutwa na bunduki ya kutengeneza kienyeji, risasi 38 za short gun, ganda moja la risasi lililotumika pamoja na mafuta ya kusafisha bunduki yaliyokuwa yamewekwa kwenye chupa ya maji ya kunywa.

 

Kamanda Sabas ambaye hakuwa tayari kutaja majina ya watu wengine watatu wanaowashikilia kwa madai kuwa bado wanaendelea kuwahoji alisema kuwa walifanikiwa kuvipata vitu hivyo  baada ya kupekuwa nyumbani kwa Pakasi.

 

"Vitu hivyo vilikuwa vimehifadhiwa kwenye mkoba mdogo uliozungushiwa kwenye mfuko mweusi wa nailoni uliokutwa ndani ya nyumba ya mtuhumiwa huyo," alisema kamanda Sabas.

 

Alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakimaliza hatua za awali za uchunguzi ambapo amewaomba wananchi kutoa taarifa polisi zitakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu.

 

MWISHO

 

huku moja ikiwa ambaye wamemk

 

Kamanda Sabas alisema kuwa Porokwa bado anaendelea na matobabu kwenye hospitali ya Seliani kwake  alipigwa risasi ya kifuani na watu waliokuwa kwenye bodaboadla  na kufariki huku mwanamke mwingine Florah Porokwa akinusurika kufaa baada ya kupigwa risasi ya kwenye mbavu ambapo alisema kuna mwanamke mwingine ambaye hakumtaja jina alipigwa risasi lakini haikumpata.

 

amefariki baada ya kupigwa risasi shingoni juzi majira ya saa 3:00 usiku wakati akihuku Florah Porokwa a

0 Comments:

Post a Comment