Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini Joseph Matare amezungumza na waandishi wa Habari na kueleza sababu za kujiuzulu wadhifa huo ili kuepusha upotoshaji unaofanywa na maadui wa Chadema.
Kiongozi huyo amesema amejiuzulu kwa sababu yeye ni mchungaji wa Kanisa la EAGT na uongozi wa Kanisa hilo umewataka wachungaji wote ambao ni viongozi katika vyama vya siasa wajiuzulu nyadhifa zote za kisiasa.
Bwana Matare amesema akiwa kama mtumishi wa Mungu alitii wito wa Kanisa na kumuandikia Rasmi Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa kumfahamisha uamuzi wake wa kujiuzulu.
Kiongozi huyo amesema anaamini kujiuzulu kwake hakutarudisha nyuma mapambano ya Chadema Kanda ya Kusini.
Ameahidi kusaidia Chadema kumpata mrithi wake ambaye ataendeleza pale alipoachia.
Kiongozi huyo amewataka wafuasi wa Chadema kote nchini kupuuza porojo zote zinazosambazwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kujiuzulu kwake.
Source:Nipashe Jumapili.
0 Comments:
Post a Comment