Al Shabab wavamia tena Pwani ya Kenya

Mashambulizi yazuka upya eneo la pwani Kenya
Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamekivamia kijiji kimoja karibu na mji wa Lamu nchini Kenya mapema leo alfajiri katika msururu wa mashambulizi ambayo yamelikumba eneo hilo la pwani katika siku za hivi karibuni.Maafisa wamesema zaidi ya washambuliaji kumi walikivamia kijiji cha Pandanguo kilichoko kilomita kiasi  arobaini kutoka mji wa Mpeketoni ambako kiasi ya watu hamsini waliuawa mwezi uliopita na kuiba bunduki za  askari wa ziada na kuzichoma nyumba na majengo mengine.Shirika la msalaba mwekundu limesema hakuna ripoti za majeruhi au waliouawa katika shambulizi hilo la leo. Miongoni mwa majengo yaliyochomwa ni pamoja na shule na zahanati huku kukiwa na ripoti kuwa wakaazi waliporwa pia mali zao. Hakuna kundi ambalo limejitokeza kudai kuhusika na mashambulizi ya wiki hii.
Source DW

0 Comments:

Post a Comment