TUKO TARAI KWENDA MAGEREZA KISONGO- NANYARO



NAIBU Meya wa jiji la Arusha, Prosper Msofe, (CHADEMA), na diwani wa kata ya Levelos, Ephata Nanyaro, (CHADEMA) wamesema kuwa wamejiandaa kukaa mahabusu  gerezani Kisongo ikiwa ni ishara ya kupinga unyanyasaji na ubambikaji kesi unaofanywa na jeshi la polisi kutokana na mashinikizo ya kisiasa.

 

Waliyasema hayo jana walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kujisalimisha kwenye kituo kituo cha kati cha polisi, Arusha kwa ajili ya kupelekwa mahakamani wakidaiwa kuwa waliwapiga mgambo wawili.

 

Nanyaro alisema kuwa wakishafikishwa mahakamani leo (jumanne) na kusomewa mashtaka hayo waliyodai kuwa ni ya kubambikwa hawatakubali dhamana ili waenda mahabusu mpaka siku nyingine ya kesi kuwafanya watawala waache kutisha watu na magereza.

 

"Sisi tulipigwa na mgambo, walitufungia "depot" (ghala) wakatuchangia, na wananchi wetu ni mashahidi kwani walikuwa nje na wao ndiyo walituita tukawasaidie kuwanusuru wenzao walionyang'anywa mali zao bila utaratibu kufuatwa kwani mgambo wamekuwa na mazoea ya kuwafungia na kuwachapa na mkia wa faru na tayari wananchi watatu wameshavunjwa miguu.

 

"Hivyo wananchi wetu wanajua ukweli kuwa baada ya sisi kuingia kule mlango ulifungwa na mgambo walituchangia tulipigwa sana kama mimi nilichanika mdomo na tulienda kutibiwa zahanati ya Ngarenaro na hospitali ya mkoa ya Mount Meru licha ya polisi kukataa kutupa PF 3.

 

"Na niweke kumbukumbu sawa, suala la sisi kukamatwa limeletwa na Mkuu wa wilaya, Arusha (John Mongela) na ni baada ya wiki iliyopita mimi kulitaka baraza la madiwani lilaani kauli yake ya kibaguzi aliyowataka machinga wanaotoka maeneo ya Babati na Moshi kurudi kwenye miji yao kama hawako tayari kufuata kanuni za jiji'" alisema Nanyaro.

 

Alisema kuwa Mkuu wa upelelezi wa wilaya, Faustine Mafwele, wametakiwa kurudi kituo hicho cha polisi leo (jumanne) saa 1.30 asubuhi kwani kesi yao bado haijasajiliwa mahakamani jambo alilowaeleza kuwa mashauri hayo usajiliwa kila siku kabla ya saa 3 asubuhi.

 

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani hapa alithibitisha kujisalimisha kwa madiwani hao ingawa hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa madai kuwa ndiyo ameingia ofisini jana asubuhi akitokea safarini nchini Israel hivyo hajaweza kupitia maifaili yote yaliyo mezani kwake.

2 comments:

  1. Hello dear mwombaji Mimi ni Mheshimiwa Stephen Brown kwa jina na i ni mmiliki wa Trust Fedha World Loan Company. Kwa heshima ya matendo yangu kubwa, mimi itabidi kama wewe kujua kwamba i kutoa kila aina ya mkopo unaweza milele kufikiria katika tu kiwango cha riba ya 3%. Harakisha sasa na kuomba kwa ajili ya mkopo wako haraka ili tuweze kupata mkopo wako mbio. Wasiliana nasi leo saa: trustfunds402@yahoo.com Omba kwa ajili ya mkopo wako leo na kupata hivyo kwa haraka kama unataka hivyo. * STEPHEN BROWN *

    ReplyDelete
  2. Habari am Bi, kiutamaduni na Tumaini, Taasisi mkopo halali na za kuaminika na mikopo
    katika sheria na masharti wazi na ya kueleweka kwa 2% kiwango cha riba. kutoka
    USD $ 12,000 kwa $ 8,000,000, Euro na paundi tu. Mimi kutoa mikopo ya biashara,
    Mikopo binafsi, mikopo ya wanafunzi, gari mikopo na mikopo kwa kulipa bili. kama wewe
    haja mkopo una kufanya ni kwa ajili ya wewe kuwasiliana nami moja kwa moja
    Katika: (merithope6@gmail.com)
    God Bless You.
    dhati,
    Bibi: sifa Hope
    Barua pepe: (merithope6@gmail.com)

    Kumbuka: majibu yote upelekwe kwa: (merithope6@gmail.com)

    ReplyDelete