Wakuu.
Kama mnavyojua kuwa kwa sasa kuna
harakati za kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa
kujaza nafasi ya Marehemu Said Bwanamdogo
kule jimbo la Chalinze, tayari mtoto wa rais
ambaye ni mgombea wa CCM kwenye jimbo
hilo ameanza kumwaga ahadi za mabilioni ya
shilingi kama jinsi alivyofanya baba yake
kwenye kampeni za urais 2010.
AHADI YA AMBULANCE
Mtoto huyo wa rais alianza kutoa ahadi ya
Ambulance akiwa Miono kata ya Mandela
ambapo ni mahali alipozikwa marehemu
Bwana mdogo. Kwa sasa kwenye jimbo hilo
wagonjwa wanao kwenda kutibiwa hospitali
ya Bagamoyo au Kibaha hupaswa kutoa
mchango wa shilingi 85,000/= kama gharama
za kugharamia mafuta ya Ambulance ambayo
niya serikali. Hii imekuwa inalalamikiwa sana
na wakazi wa jimbo hilo ambao wengi kipato
chao nicha kawaida.
Baada ya mtoto huyo wa rais kutoa ahadi ya
ambulance, watalaamu wa vifaa vya tiba na
uchunguzi wanasema ambulance iliyokamilika
kila kitu ndani kwa ajili ya kumhudumia
mgonjwa anayewahishwa kupata huduma za
ziada kwenye hospital ya wilaya au rufaa kwa
sasa ni zaidi ya shilingi milioni 100, kwaa
mana hiyo; kwa vituo vya afya zaidi ya 4
kwenye jimbo hilo itamgharimu zaidi ya
shilingi milioni 400.
AHADI YA MATREKA
Jimbo la CHALINZE lina jumla ya vijiji 86
kwenye kata 15. Bwana Ridhiwani ameshatoa
ahadi ya kununua treka kwa kila kijiji, kwa
maana hiyo atanunu matreka 86 kwa ajili ya
vijiji vyote 86 kwenye kata 15, bei ya treka
moja kwa hapa Tanzania ni zaidi ya shilingi
milioni arobaini (40 Milion). Ukichukua bei
ya treka moja 40,000,000/= x vijiji 86 =
3,440,000,000/=
Ukichukua gharama za jumla (Ambulance
zaidi milioni 400 + Matreka zaidi ya 3.4
Bilioni) unabaki kujiuliza biashara aliyofanya
kijana huyu au pesa anazotarajia kufanya
hayo yote amezipata kwenye vyanzo gani vya
mapato?! Je mapato hayo ni halali?! Anafanya
biashara gani?!
Mshahara wa mbunge pamoja na posho si
zaidi ya shilingi milioni 10, kama atabahatika
kuwa mbunge atahudumu mwaka mmoja tu
kwenye jimbo hilo kabla ya uchaguzi wa
mwaka 2015, je atakuwa amepata wapi fedha
zote hizo wakati mpaka uchaguzi mkuu ujao
kwa mshara na posho za ubunge pekee
hatakuwa hata na kiasi cha kinachozidi
shilingi milioni 500?!
Natambua kuwa mnakumbuka kuwa baba
yake aliahidi ahadi za zaidi ya shilingi 9
Trilioni ikiwa ni pamoja na kuifanya Kigoma
kuwa Dubai ya Afrika. Je hayo
yameshafanyika?
Tujikumbushe na ahadi za baba yake
kwenye kampeni za urais mwaka 2010
Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam
mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega,
Tabora
1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda -
Tanga mjini
2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria
- Igunga
3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika
mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) -
Shinyanga
4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini -
Dodoma
5. Wakulima kuacha kutumia jembe la
mkono - Dodoma mjini
6. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya
Mrijo, Dodoma
7. Wananchi kutoondolewa kwenye
Ranchi ya Misenyi - Kagera
8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi -
Kagera
9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba -
Bukoba Mjini
10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa
Kigoma - Kigoma Mjini
11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka
Uganda - Kagera
12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi,
Rukwa na Ruvuma kuunganishwa
katika gridi ya taifa ya umeme -
Kagera
13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka
mitatu - Kagera
14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya
kuua albino - Mbeya
15. Kununua meli kubwa kuliko MV
Bukoba - Kagera
16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili
ya wajasiriamali
17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika
- Mwanza
18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na
Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi
maalum chenye vifaa kupambana na
wahalifu - Mwanza
19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa
Januari mwakani - Geita
20. Kulinda muungano kwa nguvu zote -
Pemba
21. Kuwajengea nyumba waathirika wa
mafuriko Kilosa - Morogoro
22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa
Nyasa - Mbeya mjini
23. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
24. Kumaliza tatizo la walimu miaka
mitano ijayo - Songea
25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe
Kiwira - Mbeya
26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani
kuzama - Tanga
27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya
kubeba wajawazito hasa vijijini -
Iringa
28. Kujenga barabara yenye kiwango cha
lami kutoka Same mpaka Kisiwani –
Kihurio na kuiunganisha na barabara
kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same
mkoani Kilimanjaro
29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya
ya Same - Same Mjini
30. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
31. Kusambaza walimu 16,000 katika
shule za sekondari zenye upungufu
makubwa wa walimu - Kisesa Magu
32. Kununua vyandarua viwili kwa kila
kaya - Mbeya Mjini
33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu
saba nchini kuwa za rufaa ili
kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili (MHN) - Hydom
Manyara
34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia
chokochoko za kidini, kikabila na
kisiasa - Musoma
35. Kulinda haki za walemavu - Makete
36. Kujenga baabara ya Njombe - Makete
kwa kiwango cha lami,urefu wa
kilomita 109 - Iringa mjini
37. Kujenga barabara Musoma – Mto wa
Mbu Arusha - Arusha
38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu-
Shinyanga Mjini
39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-
Kigoma – Kaliua,Tabora
40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi
- Arusha Mjini
41. Kuboresha barabara ya Handeni,
Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe
waliopotea wakati wa ukame mwaka
2009 - Longido
43. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15
kutoka kwenye bomba kuu la mradi
mkuu wa maji wa Ziwa Victoria -
Shinyanga-Kahama kuunganishiwa
maji - Shinyanga
44. Tatizo la umeme kufikia kikomo
Novemba mwaka huu mkoani Arusha –
Arusha mjini
45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo -
Busekera, Wilaya ya Musoma
46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya
Longido - Longido
47. Kujenga barabara ya lami kupitia
pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya
Seregenti – Ngorongoro
48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo
ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza
kupata na kutunza mifugo yao vizuri -
Mbulu mkoani Manyara
49. Kusambaza maji nchi nzima - Babati
vijijini
50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma
za afya, na uboreshaji wa kilimo cha
umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa
wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati
vijijini
51. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi
wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo
za kilimo kwa mfumo wa vocha -
Iringa
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya
uhakika - Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda
katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha,
ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko
zote Tanzania - Iringa
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa
ujumla ili kudumisha amani na sifa ya
nchi -Ifunda
55. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda,
mkoa wa Mara
56. Kuwapa wanawake nafasi zaidi -
Kilolo, Iringa
57. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza
miradi mbalimbali ya kijamii -
Kibandamaiti Mjini Zanzibar
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi
Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa -
Kibandamaiti mjini Zanzibar
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika
msaada - Kibandamaiti
60. Serikali kujenga upya bandari ya
Mbambabay - Ruvuma
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo
wa kubeba tani 400 - Mbambabay
Ruvuma
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha
wakulima wa Mbinga (MBICU) –
Ruvuma
63. Ahadi Rais wa Marekani Barack
Obama kuimwagia misaada Tanzania –
Ruvuma
64. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa
damu baada ya uchaguzi-Dar es
Salaam
65. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –
Mtwara
66. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya
kuua viluilui vya mbu - Kibaha
67. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa -
Kibaha
68. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha
kutenga eneo maalumu la viwanda -
Kibaha
Je, ni sahihi kusema Ridhiwani ameanza
kuteswa na vinasaba vya uwongo?!
TAFAKARI
CEOrt, TWCC kushirikiana ushiriki wa wanawake katika kukuza uchumi wa
biashara
-
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Watendaji Wakuu nchini (CEO Roundtable of
Tanzania-CEOrt) B. Santina Benson (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
M...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment