Benki ya Arabuni ya Maendeleo ya Kiuchumi kwa Bara la Afrika (BADEA) imesaini mkataba wa kuikopesha Tanzania dola za Marekani milioni 23 sawa na shilingi bilioni 34.5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Wete mpaka Chakechake Pemba yenye urefu wa kilomita 22.1.
Aidha benki hiyo imetoa mkopo usio na riba wa dola za Marekani milioni 10 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 15 kwa lengo la kuharakisha zoezi la uboreshaji wa miundombinu hapa nchini ambapo fedha hizo zitaelekezwa kwenye ujenzi wa barabara hiyo.
Mkataba huo ulisainiwa jana mjini Arusha na Waziri wa fedha, William Mgimwa kwa niaba ya serikali ya Tanzania na mkurugenzi wa benki ya BADEA, Abdelaziz Khelet ambao wote wako kwenye mkutano mkuu wa benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaoendelea jijini hapa.
Waziri Mgimwa aliwashukuru Badea pamoja na Mfuko wa Saudia kutoka Uarabuni, ambao nao umetoa dola za Marekani milioni 10 sawa na shilingi bilioni 15 katika kusaidia kusaidia ujenzi wa barabara hiyo ukamilike mapema.
Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechangia dola za Marekani milioni 3 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 4.5 katika mradi huo wa barabara ambao utasaidia katika kuinua sekta ya kilimo nchini kwa kuwezesha barabara hiyo inayoelekea kwenye mashamba mengi ya karafuu.
Waziri huyo wa fedha alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu na unatarajia kukamilika Oktoba 31,2014 jambo alilodai kuwa ikikamilika itasadia kuokoa fedha za serikali ambazo zilikuwa zikitumika kukarabati mara kwa mara barabara ya kiwango cha vumbi iliyokuwepo .
Naye Waziri wa fedha wa Zanzibar, Omary Yusuph Mzee, alisema kuwa ujenzi huo utakapokamilika, utasaidia kuunganisha Mikoa miwili ya
Kusini na Kaskazini ambayo ni maarufu kwa kilimo cha karafuu na itawezesha kukuza biashara ya utalii kwenye maeneo hayo .
Kusini na Kaskazini ambayo ni maarufu kwa kilimo cha karafuu na itawezesha kukuza biashara ya utalii kwenye maeneo hayo .
0 Comments:
Post a Comment