SERIKALI KUIONGEZEA MTAJI TIB WA KATI YA DOLA MILIONI 400 NA 500



Naibu waziri wa fedha, Janeth Mbene


SERIKALI inaanzisha benki ya wakulima nchini ambayo itakuwa ikitoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu ili kuboresha sekta ya kilimo nchini ambayo ndiyo tegemeo kubwa katika kutoa ajira na kuongeza kipato cha wananchi wengi.

Aidha imekubali kuongeza mtaji kwenye benki ya rasilimali nchini (TIB) ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa fedha zitakazotumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ikiwemo ile ya uboreshaji wa miundo mbinu.

Hayo yalisemwa  na Naibu waziri wa fedha, Janeth Mbene mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 38 wa Taasisi za Benki za Maendeleo barani Afrika (AADFI) unaofanyika kwenye hoteli ya Arusha palasi ambapo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi mtendaji wa TIB, Peter Noni.

Alisema kuwa serikali imekubali kutenga kati ya dola za Marekani milioni 400 na 500 kwa ajili hiyo ambapo benki hiyo ya wakulima inatarajiwa kukamilika wakati wowote ndani ya mwaka huu kwani mchakato wake ulishaanza.




Naibu waziri wa fedha, Mbene akiwa na Mwenyekiti wa AADFI na Mkurugenzi mtendaji wa TIB, Peter Noni.


Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mbene kufungua mkutano huo Mwenyekiti wa AADFI, Noni alisema kuwa ujenzi wa majengo kwa makao makuu ya taasisi hiyo zilizoko Abidjan, Ivory Cost unaoendelea vizuri na kuwataka wanachama wa taasisi hiyo kuendelea kuchangia kama walivyokubaliana.

Akiongea kabla ya kufunguliwa warsha yao ya siku moja iliyofanyika may 29 na 30 mwaka huu , Noni ambaye pia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TIB alizitaka nchi za Afrika kuziongezea mitaji benki hizo za Maendeleo ili kuzijengea uwezo wa kuwasiliana na taasisi za fedha ndanui na nje ya nchi hivyo kuwa na fedha za kutosha kutumika kwenye uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambayo ni nguzo muhimu ya maendeleo.


Alisema kuwa suala la uboreshaji wa miundombinu kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania linahitaji kiasi kikubwa cha fedha hivyo haliwezi kufanikiwa endapo serikali zitaendelea kutegemea mikopo ya benki kubwa za kimataifa na bajeti zao pekee  badala yake zimeshauriwa kushirikiana na benki za maendeleo zilizopo kwenye nchi zao.






0 Comments:

Post a Comment