Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete zungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya washiriki 2400 toka nchi wanachama barani Afrika, Asia na Ulaya
Alitaka miundombinu barani Afrika iboreshwe ili kuwezesha a sekta ya utalii kufanya vizuri jambo litakaloongeza pato kubwa akitolea mfano nchi ya Tanzania kwa kusema kuwa kwa sasa pato kubwa linatoka katika madini na huku utalii ikiwa inashika nafasi ya pili kwa kuingiza pato kubwa
Rais wa Ivory Cost, Dk. Alassane Ouattara akiongea kwenye mkutano huo ambapo alishukuru kwa uamuzi wa kurudisha makao makuu ya AfDB kwenye mji mkuu wa nchi yake Abidjan baada ya kuhama kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na machafuko yaliyokuwa nchini mwake
Mwakilishi wa mfalme wa Morocco, akizungumza kwenye mkutano huo akishukuru kwa nchi yake kupewa fursa ya kuandaa mkutano mkuu ujao wa AfDB
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka akiongea kwenye mkutano huo alisema kuwa hazina kubwa iliyofichika kwa Afrika, sio mafuta, gesi au madini bali ni vijana .
Alizitaka serikali za Afrika kusimamia vema raslimali zilizopo ili ziweze kuleta maendeleo kwa nchi hizo, vinginevyo, raslimali hizo zitakuwa laana.
Alisema AfDB imedhamiria kuwekeza katika sekta ya miundombinu ingawa pengo la mahitaji ya fedha na mahitaji halisi ya uwekezaji katika sekta hiyo ni kubwa.
Waziri wa fedha, William Mgimwa akimnong'oneza jambo Rais Jakaya Kikwete




0 Comments:
Post a Comment