KITANDULA AWAFOKEA WAJUMBE: “MASWALI GANI HAYO MNAULIZA?”

 


TANGA, MKINGA – Mbunge wa Jimbo la Mkinga anayemaliza muda wake, Dastan Kitandula, ameonesha kukerwa na baadhi ya maswali aliyoulizwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mikutano ya kampeni ya kuomba kuteuliwa tena kugombea ubunge.

Kitandula, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, alifoka hadharani baada ya kuulizwa maswali aliyoyataja kuwa "yamepangwa" na wapinzani wake wa kisiasa, akidai kuwa yanalenga kumchafua kisiasa.

Tukio hilo lilitokea katika kata ya Daluni, wilayani Mkinga, mkoani Tanga, ambapo aliulizwa maswali matatu mfululizo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.



Jimbo la Mkinga lina wagombea sita wanaowania kuteuliwa kupitia CCM, huku ushindani mkali ukionekana kati ya Kitandula, Twaha Mwakioja na Saidi Duvii.


Kitandula  liliulizwa swali la kwanza  na mjumbe kutoka Tawi la Kisiwani A, ambaye alitaka kujua kwa nini mbunge huyo haonekani jimboni mara kwa mara kukagua miradi ya maendeleo, licha ya kutolewa kwa zaidi ya Sh bilioni 3.9 kutoka kwa Rais Samia. Kitandula alijibu kwa hasira:

“Nilijua tu lazima wewe uulize swali hilo. Ningeshangaa kama usingeuliza. Najua mmetumwa. Kama mimi naleta pesa na zinaliwa, kosa langu ni nini?”

Swali la pili lilihusu ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo, ambapo kada mmoja wa CCM alihoji kwanini kituo hicho hakijakamilika licha ya kupokea Sh milioni 500. Kitandula alijibu:

“Hapa kuna Mwenyekiti wa Kitongoji na Diwani, wao wanafanya nini? Kwa nini lawama zote mnipe mimi?”

Katika kata ya Maramba, aliulizwa kuhusu ahadi ya mwaka 2023 ya kujengwa kwa barabara ya lami ya kilomita 10, ambayo haijatekelezwa hadi sasa, huku Ilani ya Uchaguzi ya 2025–2030 ikieleza kuwa bado ipo katika hatua ya upembuzi yakinifu. Akijibu, Kitandula alisema:

“Achaneni na hao wanaosema kuhusu Ilani. Nisikilizeni mimi! Kilomita 10 zipo!”

Katika kata ya Kigongo Magharibi, mjumbe mwingine alimkumbusha kuwa mbunge aliyemtangulia, Mwandoro, alikaa miaka 10 na barabara ilikuwa inapitika vizuri, lakini hali hiyo imekuwa mbaya tangu Kitandula aingie madarakani. Kitandula alijibu kwa ukali:

“Msipende kutengenezewa maswali. Hata kama mkipewa maswali, yawekeni vizuri ili isionekane ni ya kutungwa.”

Hata hivyo, aliwahakikishia wajumbe kuwa serikali itaweka barabara za zege katika maeneo ya milimani ili kutatua changamoto ya barabara mbovu.

Jimbo la Mkinga lina wagombea sita wanaowania kuteuliwa kupitia CCM, huku ushindani mkali ukionekana kati ya Kitandula, Twaha Mwakioja na Saidi Duvii.

0 Comments:

Post a Comment