Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameonekana hadharani leo, Machi 25, 2025, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu.
Mbowe alihudhuria msiba wa Wilfred Joachim Ngure, baba mkwe wa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye alifariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mbowe ameungana na waombolezaji wengine kutoa pole kwa familia ya Mwigulu.
Baada ya ibada hiyo, msafara wa mazishi umeelekea Shia, Old Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko.
Kuonekana kwa Mbowe kwenye tukio hili kumewavutia wengi, kutokana na muda mrefu kuwa kimya kwenye masuala ya siasa.
0 Comments:
Post a Comment