Katika maelezo yake, Museveni alisema kuwa ni muhimu kuwa na uwajibikaji katika utawala, na akataka watu kuelewa kuwa suala la kisiasa linapaswa kutolewa pembeni ili haki itendeke. Alisema, "Nimeona wasiwasi wa Waganda juu ya kuzuiliwa kwa Dk. Besigye kwa makosa makubwa ambayo anadaiwa alikuwa amepanga."
Rais alieleza kuwa swali la msingi linapaswa kuwa: "Kwa nini Dk. Besigye alikamatwa?" Aliongeza kwamba, "Jibu la hilo ni kesi yake imalizwe kwa haraka ili ukweli ujitokeze." Kwa mujibu wa Museveni, kucheleweshwa kwa kesi hiyo kunachochea ukosefu wa usalama na kudhuru uthabiti wa nchi.
Aidha, Rais Museveni alizungumza kuhusu hali ya kiafya ya Dr. Besigye, akisema kuwa kuna hospitali ya umma katika gereza na wahudumu wa afya wa kibinafsi wanatembelea kiongozi huyo wa upinzani. Alisema kuwa ikiwa kuna haja ya huduma ya ziada ya matibabu, serikali itafanya uchunguzi na kutoa ushauri. Alijikita pia kwenye suala la mgomo wa kutokula wa Besigye, akidai kuwa hali ya dhaifu aliyokuwa nayo ni kutokana na hatua yake hiyo: "Katika hili, Dk Besigye, alikuwa kwenye mgomo wa kutokula. Hiyo ni sehemu ya sababu ya yeye kuwa dhaifu kunakoonekana kwenye picha zilizoko magazeti. Je! huo sio ulaghai usio na msingi?"
Maelezo ya Rais Museveni yanakuja baada ya familia ya Dr. Besigye kuibua wasiwasi kuhusu hali ya afya ya kiongozi huyo, ikieleza kuwa idara ya magereza ya Uganda iliitaka familia hiyo kutuma daktari binafsi wa Besigye.
Mbunge wa Buhweju, Francis Mwijukye, alielezea kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba Dr. Besigye, ambaye alikuwa akitumia kiti cha magurudumu, alipelekwa hospitali iliyoko katika jengo la kibiashara la Bugolobi Village Mall.
Kwa upande mwingine, Rais Museveni alizungumzia hatua ya kuhama kwa kesi ya Dr. Besigye kutoka Mahakama ya Kijeshi hadi Mahakama za Kiraia, akisema, "Ni nani anayechelewsha kesi? Mahakama ndio uliogundua mapungufu katika mahakama ya kijeshi na wakaagiza kuhamishwa kwa kesi hiyo hadi Mahakama za Kiraia."
Dr. Kizza Besigye, ambaye alikuwa daktari binafsi wa Rais Museveni, alikamatwa katika mazingira ya kutatanisha mwezi Novemba mwaka jana jijini Nairobi pamoja na msaidizi wake wa kisiasa, Obeid Lutale. Alikamatwa kwa tuhuma za kumiliki silaha na kusomewa mashtaka katika mahakama ya kijeshi.
Soma Zaidi;
https://habaritanzaniagracemacha.blogspot.com/2025/02/kizza-besigye-akimbizwa-hospitali-baada.html
0 Comments:
Post a Comment