Trump aapishwa rasmi, aelezea changamoto za taifa

 


Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, pamoja na makamu wake mteule JD Vance, wameapishwa rasmi kuwa Rais na Makamu wa Rais wa 47 wa taifa la Marekani katika hafla ya kihistoria. 



Trump, ambaye alishinda katika uchaguzi wa rais, sasa anakuwa Rais wa 47 wa Marekani huku JD Vance akiwa Makamu wa Rais.


Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Trump alizungumzia masuala mengi yanayohusiana na hali ya taifa la Marekani na changamoto kubwa zinazokikabili. 


Alianza kwa kutoa maoni yake kuhusu hali ya afya na elimu nchini, akisisitiza kuwa kuna mabadiliko makubwa yatakayofanyika kwa haraka.


Trump alisema,

"Marekani ina mfumo wa afya ambao hautoi wakati wa maafa, lakini pesa nyingi zinatumika kwa hilo kuliko popote duniani."


Alielezea kuwa mfumo wa elimu nchini Marekani unafundisha watoto kujionea aibu, na kwamba hali hiyo itabadilika kwa haraka.



"Nchi ina mfumo wa elimu ambao unafundisha watoto wetu kujionea aibu," alisema Trump.



Pia, alishambulia utawala wa Rais Joe Biden, akieleza kuwa changamoto kubwa zinazokikabili taifa la Marekani, ikiwa ni pamoja na mizozo ya kiuchumi na kijamii, zitashughulikiwa haraka na kwa ufanisi. 


Alikosoa utawala wa awamu iliyopita kwa kile alichokiita kutoa ulinzi kwa wahalifu hatari kutoka nje ya Marekani huku ukikosa kutatua changamoto za ndani ya nchi.


"Sasa tuna serikali ambayo haiwezi kudhibiti hata shida rahisi nyumbani," alisema Trump akizungumza kuhusu hali ya sasa ya utawala wa Marekani.


Aidha, Trump alizungumzia suala la wahamiaji, akisema kuwa utawala wa Biden umefanya makosa makubwa katika kudhibiti mipaka ya Marekani na kutoa hifadhi kwa wahalifu hatari. 


Aliongeza kuwa utawala wa zamani umekuwa ukipeleka msaada mkubwa kwa mipaka ya kigeni, lakini unapuuza kulinda mipaka ya Marekani.



Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Trump alizungumzia kuhusu jaribio la mauaji dlĺĺĺ0cha miaka minane alikumbana na jaribio la kuwaondoa madarakani zaidi ya viongozi wengine wa zamani wa Marekani. 


Aliendelea kusema kuwa jaribio hilo lilikuwa sehemu ya mbinu za kumzuia kutoka kuendelea na kazi yake ya kutimiza malengo yake ya kulifanya taifa la Marekani kuwa bora tena.


"Wamejaribu kusimamisha kazi yetu na kujaribu kuchukua uhuru wangu, na kwa kweli maisha yangu," alisema Trump, akiongeza kuwa maisha yake yaliokolewa kwa sababu ya kauli mbiu yake ya kampeni ya "kuifanya Marekani kuwa bora tena".



Trump pia alizungumzia kimbunga kilichotokea huko North Carolina na moto wa Los Angeles, akisema kuwa madhara ya moto huo yameathiri baadhi ya matajiri na wenye nguvu zaidi, na kuonyesha kuwa mataifa yanafaa kujizatiti katika kukabiliana na majanga na maafa.


"Hawana nyumba tena," alisema Trump akiwaeleza hadhira ya Capitol Rotunda, na kusema kuwa Marekani inahitaji mfumo wa afya bora, na mfumo wa elimu utakaowaandaa vijana kwa ajili ya mustakabali bora.


Hii ni hafla muhimu katika historia ya Marekani na inadhihirisha kuanza kwa utawala mpya chini ya Rais Donald Trump, ambaye ameahidi kuchukua hatua za haraka na za maana katika kuboresha hali ya taifa.

0 Comments:

Post a Comment