Mama na Mtoto Walawitiwa na Kuuawa

Mama na Mtoto Walawitiwa na Kuuawa



Watu wasiojulikana wanadaiwa kuwalawiti na kuwachoma na kitu chenye ncha kali mama na mtoto wake katika mtaa wa Muungano, Kata ya Mkonze Jijini Dodoma. Tukio hili la kikatili limetokea usiku wa kuamkia Alhamisi tarehe 06 Septemba 2024.


Mashuhuda ambao ni majirani wa eneo hilo wamesema kuwa mama huyo anayefahamika kwa jina la Mwavita Mwakibasi (33), na binti yake Salma Silvesta (11), walikutwa wamefariki wakiwa na majeraha mabaya sehemu mbalimbali za miili yao ndani ya nyumba yao.


Mtoto mkubwa wa marehemu, ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema kwa uchungu kuwa aliamshwa na mdogo wake na kumweleza kuwa mama yao alikuwa akivuja damu. 


Hali hiyo ilimlazimu kupiga simu kwa bibi yao ili waweze kupata msaada wa haraka. Dada wa marehemu alisema alipata taarifa za tukio hilo kupitia simu ya mama yao aliyepo Mbeya.


Mwenyekiti wa mtaa huo amelaani vikali kitendo hicho na kusema, “Tunaiomba serikali na Jeshi la Polisi kuweka kituo cha polisi katika eneo hili ambalo linakua kwa kasi, ili kusaidia kukabiliana na vitendo vya kikatili vinavyoongezeka."


Lazaro Mbishe, Kaimu Kitengo cha Mawasiliano katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, amethibitisha kupokea miili ya marehemu na kuongeza kuwa mtoto ambaye alikua mahututi alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.


Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili lenye kuhuzunisha.

0 Comments:

Post a Comment