Leo, Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), chini ya uongozi wa Mwenyekiti Jenerali (Mst) George Waitara, imefanya ziara muhimu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Ziara ililenga kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za uhifadhi na maendeleo katika eneo hili adimu la urithi wa dunia.
Bodi ilipata fursa ya kukagua hali ya hifadhi, mipango ya uhifadhi endelevu, na kujadili mikakati ya kuendeleza utalii na uhifadhi wa maliasili pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa hifadhi.
TANAPA inaendelea kujizatiti katika kulinda na kuhifadhi urithi wetu wa kitaifa kwa vizazi vijavyo.
0 Comments:
Post a Comment