Watoto Milioni 181 Wanaokabiliwa na Umaskini Mkubwa wa Chakula - Ripoti ya UNICE

 Watoto Milioni 181 Wanaokabiliwa na Umaskini Mkubwa wa Chakula - Ripoti ya UNICE



Ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) imebainisha kuwa mtoto mmoja kati ya wanne mwenye umri chini ya miaka mitano anakabiliwa na umaskini mkubwa wa chakula, huku asilimia 27 ya watoto hao wakipata milo isiyozidi miwili kati ya minane inayotambuliwa na UNICEF. Hali hii inawaweka katika hatari kubwa ya kukumbwa na utapiamlo unaotishia maisha yao.


Kulingana na ripoti hiyo, zaidi ya theluthi mbili ya watoto wanaokabiliwa na umaskini mkali wa chakula wanaishi katika maeneo ya Asia Kusini na kusini mwa Jangwa la Sahara. Nchi 20 zinatajwa kuwa na asilimia 65 ya watoto wanaokabiliwa na hali hii.


Mtaalamu wa UNICEF, Harriet Torlesse, amebainisha kuwa uzito dhaifu wa mwili kati ya watoto unaweza kusababisha hatari kubwa, huku akiongeza kuwa kuna uwezekano wa mara 12 wa kufariki kutokana na hali hiyo.


Hali ya umaskini wa chakula imekuwa mbaya zaidi katika maeneo kama Gaza, ambapo vita vya Israel dhidi ya Hamas vimeongeza mateso kwa watoto na familia zao.


Ripoti hii ya UNICEF inatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa watoto wote, ili kuzuia athari za umaskini mkubwa wa chakula ambazo zinaweza kuwa na madhara ya kudumu kwa maisha na afya ya watoto duniani kote.

0 Comments:

Post a Comment