Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa Zanzibar na Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu-UAE.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipokutana na Ali Rashid Alnuaimi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya UAE.
Dk Mwinyi amefurahishwa na wawekezaji wanaounga mkono miradi mbalimbali Zanzibar wakiwemo Wafanyabiashara kutoka UAE.
Aidha, amemweleza Alnuaimi kuwashajihisha Wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini.




0 Comments:
Post a Comment