Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda, amefariki dunia katika ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Njia Panda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa kwenye ziara mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo, Juni 18, 2024, na kusema kuwa ajali hiyo imetokea kati ya saa 8 na saa 9 mchana. "Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali," amesema RC Babu.
Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, marehemu Nzunda alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia, inadaiwa kuwa dereva wake amefariki dunia katika ajali hiyo.
Habari zaidi kuhusu ajali hii zitafuatia kadri tunavyopokea taarifa mpya.



0 Comments:
Post a Comment